Revelation 4:5 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Umeme, sauti na ngurumo, vilikuwa vinatoka kwenye hicho kiti cha enzi. Taa saba za moto zilikuwa zinawaka mbele ya hicho kiti cha enzi. Taa hizo ni roho saba za Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwenye kile kiti cha enzi palikuwa panatoka miali ya radi, ngurumo na sauti za radi. Mbele ya kiti cha enzi, taa saba zilikuwa zinawaka. Hizi ndizo roho saba za Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na sauti na ngurumo. Na taa saba za moto zilikiwaka mbele ya kile kiti cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mianga na ngurumo za radi vilitoka katika kiti cha enzi. Mbele ya kiti cha enzi zilikuwepo taa saba zikiwaka, ambazo ndizo Roho saba za Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Umeme, sauti na ngurumo, vilikuwa vinatoka kwenye hicho kiti cha enzi. Taa saba za moto zilikuwa zinawaka mbele ya hicho kiti cha enzi. Taa hizo ni roho saba za Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Umeme, sauti na ngurumo, vilikuwa vinatoka kwenye hicho kiti cha enzi. Taa saba za moto zilikuwa zinawaka mbele ya hicho kiti cha enzi. Taa hizo ni roho saba za Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwenye kile kiti cha enzi palikuwa panatoka miali ya umeme wa radi, ngurumo na sauti za radi. Mbele ya hicho kiti cha enzi, palikuwa na taa saba zilizokuwa zinawaka. Hizi ndizo Roho saba za Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwenye kile kiti cha enzi palikuwa panatoka miali ya umeme wa radi, ngurumo na sauti za radi. Mbele ya kiti cha enzi, taa saba zilikuwa zinawaka. Hizi ndizo roho saba za Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na sauti na ngurumo. Na taa saba za moto zikiwaka mbele ya kile kiti cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Umeme, sauti na ngurumo, vilikuwa vinatoka kwenye hicho kiti cha enzi. Taa saba za moto zilikuwa zinawaka mbele ya hicho kiti cha enzi. Taa hizo ni roho saba za Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo penye kiti cha kifalme palipiga umeme na vivumo na ngurumo, tena palikuwa na mienge saba ya moto iliyowaka mbele ya kiti cha kifalme, ndio zile roho saba za Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na sauti na ngurumo. Na taa saba za moto zilikiwaka mbele ya kile kiti cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Umeme ulipiga tokea katika kiti kile, na makelele na ngurumo ya radi vilisikilika. Mbele ya kiti kile kulikuwa kukiwaka mienge saba, na hizo ndizo zile roho saba za Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na ngurumo na sauti. Na taa saha za moto zikiwaka mbele ya kiti kile cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu.