Revelation 4:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mbele ya kiti cha enzi kulikuwa na kitu kama bahari ya kioo, angavu kama jiwe ling'aalo sana. Katika pande zote za hicho kiti cha enzi na kukizunguka, kulikuwa na viumbe hai wanne. Viumbe hao walikuwa wamejaa macho mbele na nyuma.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia mbele ya kiti cha enzi palikuwa na kile kilichoonekana kama bahari ya kioo, iliyokuwa angavu kama bilauri. Katikati, kukizunguka kile kiti cha enzi, kulikuwa na viumbe wanne wenye uhai, wamejaa macho mbele na nyuma.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Pia mbele ya kiti cha enzi kilikuwepo kitu kilichoonekana kama bahari ya kioo, iiliyo angavu sana. Mbele ya kiti cha enzi na kukizunguka pande zake zote walikuwepo viumbe wenye uhai wanne. Walikuwa na macho kila mahali.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mbele ya kiti cha enzi kulikuwa na kitu kama bahari ya kioo, angavu kama jiwe linga'aalo sana. Katika pande zote za hicho kiti cha enzi na kukizunguka, kilikuwa na viumbe hai vinne. Viumbe hivyo vilikuwa vimejaa macho mbele na nyuma.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mbele ya kiti cha enzi kulikuwa na kitu kama bahari ya kioo, angavu kama jiwe ling'aalo sana. Katika pande zote za hicho kiti cha enzi na kukizunguka, kulikuwa na viumbe hai wanne. Viumbe hao walikuwa wamejaa macho mbele na nyuma.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia mbele ya hicho kiti cha enzi palikuwa na kile kilichoonekana kama bahari ya kioo, iliyokuwa angavu kama jiwe lisilo na rangi yo yote ling'aalo sana. Katikati, kukizunguka kile kiti cha enzi, kulikuwa na viumbe wanne wenye uhai, wakiwa wamejawa na macho mbele na nyuma.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia mbele ya kiti cha enzi palikuwa na kile kilichoonekana kama bahari ya kioo, iliyokuwa angavu kama bilauri. Katikati, kukizunguka kile kiti cha enzi, kulikuwa na viumbe wanne wenye uhai, wakiwa wamejawa na macho mbele na nyuma.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mbele ya kiti cha enzi kulikuwa na kitu kama bahari ya kioo, angavu kama jiwe ling'aalo sana. Katika pande zote za hicho kiti cha enzi na kukizunguka, kulikuwa na viumbe hai wanne. Viumbe hao walikuwa wamejaa macho mbele na nyuma.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena mbele ya kiti cha kifalme kulikuwako yenye mfano wa bahari ya kioo iliyofanana na ulanga uangazikao. Napo katikati penye kiti cha kifalme na kukizunguka kiti cha kifalme palikuwa na nyama wanne waliojaa macho mbele na nyuma.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena mbele ya kiti kile kulionekana kama bahari ya kioo, kulingaa sana kama kilauri. Kile kiti cha kifalme kilikuwa kimezungukwa pande zote na viumbe vine vya ajabu, vyenye kujaa macho mbele na nyuma.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na mliele ya kile kiti cha enzi, mfano wa bahari ya kioo eheupe, kama krustallo, na kati kati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, nyama wane, wamejaa macho mbele na nyuma.