Revelation 4:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kiumbe wa kwanza alikuwa kama simba, wa pili kama ng'ombe, wa tatu alikuwa na sura ya mtu, na wa nne alikuwa kama tai anayeruka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kiumbe wa kwanza mwenye uhai alikuwa kama simba, wa pili alikuwa kama ng’ombe dume, wa tatu alikuwa na uso kama wa mwanadamu, na wa nne alikuwa kama tai anayeruka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na huyo mwenye uhai wa kwanza alikuwa mfano wa simba; na mwenye uhai wa pili alikuwa mfano wa ndama; na mwenye uhai wa tatu alikuwa na uso kama uso wa mwanadamu; na mwenye uhai wa nne alikuwa mfano wa tai arukaye.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kiumbe wa kwanza alikuwa kama simba. Wa pili alikuwa kama fahali. Wa tatu alikuwa na uso kama wa mwanadamu. Wa nne alikuwa kama tai anayeruka.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kiumbe cha kwanza kulikuwa kama simba, cha pili kama ng'ombe, cha tatu kilikuwa na sura kama mtu, na cha nne kilikuwa kama tai anayeruka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kiumbe wa kwanza alikuwa kama simba, wa pili kama ng'ombe, wa tatu alikuwa na sura ya mtu, na wa nne alikuwa kama tai anayeruka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huyo kiumbe wa kwanza mwenye uhai alikuwa kama simba, wa pili alikuwa kama ng'ombe dume, wa tatu alikuwa na uso kama wa mwanadamu na wa nne alikuwa kama tai anayeruka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kiumbe wa kwanza mwenye uhai alikuwa kama simba, wa pili alikuwa kama ng’ombe dume, wa tatu alikuwa na uso kama wa mwanadamu, na wa nne alikuwa kama tai anayeruka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na huyo mwenye uhai wa kwanza alikuwa mfano wa simba; na mwenye uhai wa pili alikuwa mfano wa ndama; na mwenye uhai wa tatu alikuwa na uso kama uso wa mwanadamu; na mwenye uhai wa nne alikuwa mfano wa tai arukaye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kiumbe wa kwanza alikuwa kama simba, wa pili kama ng'ombe, wa tatu alikuwa na sura ya mtu, na wa nne alikuwa kama tai anayeruka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nyama wa kwanza alifanana na simba, nyama wa pili alifanana na dume la ng'ombe, nyama wa tatu alikuwa na uso kama wa kimtu, nyama wa nne alifanana na tai mwenye kuruka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na huyo mwenye uhai wa kwanza alikuwa mfano wa simba; na mwenye uhai wa pili alikuwa mfano wa ndama; na mwenye uhai wa tatu alikuwa na uso kama uso wa mwanadamu; na mwenye uhai wa nne alikuwa mfano wa tai arukaye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kiumbe cha kwanza kilifanana na simba, kiumbe cha pili kilifanana na mwana-ngombe na kiumbe cha tatu kilifanana na mutu na kiumbe cha ine kilifanana na tai anayeruka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na nyama wa kwanza alikuwa mfano wa simba, na nyama wa pili mfano wa ndama, na nyama wa tatu mwenye nso kama uso wa Mwana Adamu, na nyama wa nne mfano wa tai arukae.