Revelation 4:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Viumbe hao wanne walikuwa na mabawa sita kila mmoja, na walikuwa wamejaa macho, ndani na nje. Usiku na mchana, bila kupumzika, huimba: “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, Bwana, Mungu Mwenye Nguvu, aliyekuwako, aliyeko na anayekuja!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila mmoja wa hawa viumbe wanne wenye uhai alikuwa na mabawa sita, na kujawa na macho pande zote hadi chini ya mabawa. Usiku na mchana hawaachi kusema: “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako, aliyeko, na atakayekuja.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hawa wenye uhai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita; na pande zote na ndani wamejaa macho, wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kila mmoja wa hawa wenye uhai wanne alikuwa na mabawa sita. Walikuwa na macho kila mahali, ndani na nje. Usiku na mchana hawaachi kusema: “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu ni Bwana Mungu Mwenye nguvu zote. Daima amekuwepo, yupo na anakuja.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Viumbe hivyo vinne vilikuwa na mabawa sita kila kimoja, na vilikuwa vimejaa macho, ndani na nje. Usiku na mchana, bila kupumzika huimba: “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu ni Bwana, Mungu Mwenye Uwezo, aliyekuwako, aliyeko na anayekuja!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Viumbe hao wanne walikuwa na mabawa sita kila mmoja, na walikuwa wamejaa macho, ndani na nje. Usiku na mchana, bila kupumzika, huimba: “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, Bwana, Mungu Mwenye Nguvu, aliyekuwako, aliyeko na anayekuja!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila mmoja wa hawa viumbe wenye uhai wanne, alikuwa na mabawa sita na kujawa na macho pande zote, hadi chini ya mabawa. Usiku na mchana hawakuacha kusema: “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni BWANA Mungu Mwenyezi, aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila mmoja wa hawa viumbe wanne wenye uhai alikuwa na mabawa sita, na kujawa na macho pande zote hadi chini ya mabawa. Usiku na mchana hawaachi kusema: “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni bwana Mwenyezi Mungu, aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hawa wenye uhai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita; pande zote na ndani wamejaa macho, wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Viumbe hao wanne walikuwa na mabawa sita kila mmoja, na walikuwa wamejaa macho, ndani na nje. Usiku na mchana, bila kupumzika, huimba: “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, Bwana, Mungu Mwenye Nguvu, aliyekuwako, aliyeko na anayekuja!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kila mmoja wao hao nyama wanne alikuwa na mabawa sita yaliyojaa macho po pote, nje ndani; hawapumziki mchana wala usiku wakisema: Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu ni Bwana Mungu, yeye Mwenyezi aliyekuwapo, aliopo, atakayekuja.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hawa wenye uhai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita; na pande zote na ndani wamejaa macho, wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kila kimoja cha viumbe vya ajabu kilikuwa na mabawa sita yenye kujaa macho ndani na inje. Navyo viliimba muchana na usiku bila kuchoka, vikisema: “Mutakatifu, mutakatifu, mutakatifu ni Bwana wetu, Mungu Mwenye Uwezo, aliyekuwa, anayekuwa na anayekuja.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na hawa nyama wane, wenye uhayi, killa mmoja alikuwa na mabawa sita: pande zote na ndani wamejaa macho, nao hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyiezi, aliyekuwako, nae yuko, nae anakuja.