Revelation 5:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nikasikia viumbe vyote mbinguni, duniani, chini ya dunia na baharini — viumbe vyote ulimwenguni — vikisema: “Kwake yeye aketiye katika kiti cha enzi, na kwa Mwanakondoo, iwe sifa na heshima na utukufu na enzi, milele na milele.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha nikasikia kila kiumbe mbinguni na duniani, chini ya nchi, na baharini, na vyote vilivyomo, vikiimba: “Sifa na heshima na utukufu na uweza ni vyake yeye aliyeketi juu ya hicho kiti cha enzi, na kwa Mwana-Kondoo, milele na milele!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndipo nikasikia kila kiumbe kilichoumbwa kilichoko mbinguni na duniani na chini ya dunia na baharini, viumbe vyote sehemu hizo vikisema: “Sifa zote na heshima na utukufu na nguvu kuu ni kwa ajili yake Yeye aketiye kwenye kiti cha enzi na kwa Mwanakondoo milele na milele!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nikasikia viumbe vyote mbinguni, duniani, chini kuzimuni na baharini—viumbe vyote ulimwenguni—vikisema: “Kwake yeye aketiye katika kiti cha enzi, na kwa Mwanakondoo, iwe sifa na heshima na utukufu na enzi milele na milele.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nikasikia viumbe vyote mbinguni, duniani, chini ya dunia na baharini — viumbe vyote ulimwenguni — vikisema: “Kwake yeye aketiye katika kiti cha enzi, na kwa Mwanakondoo, iwe sifa na heshima na utukufu na enzi, milele na milele.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha nikasikia kila kiumbe mbinguni na duniani, chini ya nchi na baharini na vyote vilivyomo ndani yake vikiimba: “Sifa na heshima na utukufu na uweza ni vyake yeye aketiye juu ya hicho kiti cha enzi na kwa Mwana-Kondoo, milele na milele!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha nikasikia kila kiumbe mbinguni na duniani, chini ya nchi na baharini na vyote vilivyomo ndani yake vikiimba: “Sifa na heshima na utukufu na uweza ni vyake yeye aketiye juu ya hicho kiti cha enzi na kwa Mwana-Kondoo, milele na milele!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi na juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nilivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na kwake Mwana-kondoo, hata milele na milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nikasikia viumbe vyote mbinguni, duniani, chini ya dunia na baharini – viumbe vyote ulimwenguni – vikisema: “Kwake yeye aketiye katika kiti cha enzi, na kwa Mwanakondoo, iwe sifa na heshima na utukufu na enzi, milele na milele.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Navyo viumbe vyote vilivyoko mbinguni, navyo vilivyopo nchini, navyo vilivyoko kuzimuni, navyo vilivyomo baharini, navyo vyote vilivyomo ndani yao, nikavisikia, vikisema: Mpeni yeye aliyekaa kitini mwa kifalme naye Mwana kondoo mapongezo na heshima na utukufu na nguvu kale na kale pasipo mwisho!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nikasikia vilevile viumbe vyote vinavyokuwa mbinguni, katika dunia, katika kuzimu na vile vinavyokuwa katika bahari; viumbe vyote vya ulimwengu nzima vikimwimbia: “Utukufu, heshima, sifa na nguvu milele na milele, kwa yule anayeikaa juu kiti cha kifalme na kwa Mwana-Kondoo.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na killa kiumbe kilicho mbinguni na juu ya inchi na chini ya inchi na juu ya bahari, na vitu vyote vilivyo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na una Mwana Kondoo hatta milele na milele.