Revelation 5:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na wale viumbe hai wanne wakasema, “Amina!” Na wale wazee wakaanguka kifudifudi, wakaabudu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale viumbe wenye uhai wanne wakasema, “Amen!” Nao wale wazee wakaanguka kifudifudi wakaabudu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee wakaanguka, wakasujudu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Viumbe wenye uhai wanne wakasema, “Amina!” Na wazee wakainama chini wakasujudu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Na vile viumbe vinne hai vikasema, “Amina!” Na wale wazee wakaanguka kifudifudi, wakaabudu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na wale viumbe hai wanne wakasema, “Amina!” Na wale wazee wakaanguka kifudifudi, wakaabudu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale viumbe wenye uhai wanne wakasema, “Amen!” Nao wale wazee ishirini na wanne wakaanguka kifudifudi wakaabudu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale viumbe wenye uhai wanne wakasema, “Amen!” Nao wale wazee ishirini na wanne wakaanguka kifudifudi wakaabudu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee wakaanguka, wakasujudu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na wale viumbe hai wanne wakasema, “Amina!” Na wale wazee wakaanguka kifudifudi, wakaabudu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wale nyama wanne waliposema: Amin, ndipo, wale wazee walipoanguka chini, wakamsujudia mwenye kuishi kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee wakaanguka, wakasujudu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vile viumbe vine vya ajabu vilijibu: “Amina.” Na wale wazee wakainama uso mpaka chini na kuabudu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na wale nyama wane wenye uhayi wakasema, Amin. Na wale wazee ishirini na wane wakaanguka wakamsujudu yeye aliye hayi milele na milele.