Revelation 5:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wakaimba wimbo huu mpya: “Wewe wastahili kukitwaa hicho kitabu na kuivunja mihuri yake. Kwa sababu wewe umechinjwa, na kwa damu yako umemnunulia Mungu wetu watu kutoka kila kabila, lugha, jamaa na taifa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nao wakaimba wimbo mpya, wakisema: “Wewe unastahili kukitwaa kitabu na kuivunja mihuri yake, kwa sababu ulichinjwa, na kwa damu yako ukamnunulia Mungu watu kutoka kila kabila, kila lugha, kila jamaa na kila taifa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na wote walimwimbia wimbo mpya Mwanakondoo: “Unastahili kukichukua kitabu na kuifungua mihuri yake, kwa sababu uliuawa, na kwa sadaka ya damu yako uliwanunua watu kwa ajili ya Mungu, kutoka kila kabila, lugha, rangi na taifa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, wakaimba wimbo huu mpya: “Wewe unastahili kukitwaa hicho kitabu na kuivunja mihuri yake. Kwa sababu wewe umechinjwa, na kwa damu yako umemnunulia Mungu watu kutoka katika kila kabila, lugha, jamaa na taifa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wakaimba wimbo huu mpya: “Wewe wastahili kukitwaa hicho kitabu na kuivunja mihuri yake. Kwa sababu wewe umechinjwa, na kwa damu yako umemnunulia Mungu wetu watu kutoka kila kabila, lugha, jamaa na taifa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nao wakaimba wimbo mpya, wakisema: “Wewe unastahili kukitwaa kitabu na kuzivunja lakiri zake, kwa sababu ulichinjwa na kwa damu yako ukamnunulia Mungu watu kutoka katika kila kabila, kila lugha, kila jamaa na kila taifa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nao wakaimba wimbo mpya, wakisema: “Wewe unastahili kukitwaa kitabu na kuzivunja lakiri zake, kwa sababu ulichinjwa na kwa damu yako ukamnunulia Mungu watu kutoka kila kabila, kila lugha, kila jamaa na kila taifa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuifungua mihuri yake; kwa kuwa ulichinjwa, ukawa fidia kwa Mungu na kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wakaimba wimbo huu mpya: “Wewe wastahili kukitwaa hicho kitabu na kuivunja mihuri yake. Kwa sababu wewe umechinjwa, na kwa damu yako umemnunulia Mungu wetu watu kutoka kila kabila, lugha, jamaa na taifa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wakaimba wimbo mpya wakisema: Wewe umepaswa na kukipokea kitabu na kuziondoa muhuri zake, kwani umechinjwa, umkombolee Mungu kwa damu yako watu wa mashina yote na wa misemo yote na wa makabila yote na wa wamizimu wote,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao walikuwa wakiimba wimbo huu mupya wakisema: “Wewe unastahili kukamata kizingo cha karatasi, na kuvunja vifundo vya mihuri yake. Kwa sababu wewe uliuawa, na kwa njia ya damu yako, ulikomboa kwa ajili ya Mungu watu wa kila kabila, wa kila luga, wa kila jamaa na wa kila taifa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nao waimba uimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulicbinjwa