Revelation 6:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, nikamwona Mwanakondoo anavunja mhuri mmojawapo wa ile mihuri saba. Nikasikia mmoja wa wale viumbe hai wanne akisema kwa sauti kama ya ngurumo, “Njoo!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nikaangalia Mwana-Kondoo alipofungua ule muhuri wa kwanza miongoni mwa mihuri saba. Ndipo nikasikia mmoja wa wale viumbe wanne wenye uhai akisema kwa sauti kama ya radi: “Njoo!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha nikaona napo Mwana-Kondoo alipofungua moja ya zile muhuri saba, nikasikia mmoja wa wale wenye uhai wanne akisema, kama kwa sauti ya ngurumo, Njoo!
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha nilitazama Mwanakondoo alipokuwa anaufungua muhuri wa kwanza kati ya mihuri saba. Kisha nikasikia sauti ya mmoja wa viumbe wenye uhai wanne akisema kwa sauti kama ngurumo ya radi ikisema, “Njoo!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha nikamwona Mwanakondoo anavunja mhuri mmojawapo wa ile mihuri saba. Nikasikia kimoja cha vile viumbe hai vinne kikisema kwa sauti kama ya ngurumo, “Njoo!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, nikamwona Mwanakondoo anavunja mhuri mmojawapo wa ile mihuri saba. Nikasikia mmoja wa wale viumbe hai wanne akisema kwa sauti kama ya ngurumo, “Njoo!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha nikaangalia wakati Mwana-Kondoo akivunja ile lakiri ya kwanza miongoni mwa zile saba. Ndipo nikasikia mmoja wa wale viumbe wenye uhai wanne akisema kwa sauti kama ya radi: “Njoo!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha nikaangalia wakati Mwana-Kondoo akivunja ile lakiri ya kwanza miongoni mwa zile saba. Ndipo nikasikia mmoja wa wale viumbe wanne wenye uhai akisema kwa sauti kama ya radi: “Njoo!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha nikaona Mwana-kondoo alipofungua mojawapo ya ile mihuri saba, nikasikia mmoja wa wale wenye uhai wanne akisema, kama kwa sauti ya ngurumo, Njoo!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, nikamwona Mwanakondoo anavunja mhuri mmojawapo wa ile mihuri saba. Nikasikia mmoja wa wale viumbe hai wanne akisema kwa sauti kama ya ngurumo, “Njoo!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha nikamwona Mwana kondoo, akifungua moja ya zile muhuri saba. Nikasikia, mmoja wa wale nyama wanne akisema kama kwa sauti ya ngurumo: Njoo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha nikaona napo Mwana-Kondoo alipofungua moja ya zile muhuri saba, nikasikia mmoja wa wale wenye uhai wanne akisema, kama kwa sauti ya ngurumo, Njoo!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha nikaona mambo haya: Mwana-Kondoo alipofungua kifundo cha muhuri wa kwanza kati ya ile mihuri saba, nikasikia kimoja kati ya vile viumbe vya ajabu kikisema hivi kwa sauti kama ya ngurumo ya radi: “Kuja!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
NIKAONA hapo Mwana Kondoo alipofungua moja ya zile muhuri, nikasikia mmoja wa wale nyama wenye uhayi akisema, kama sauti ya ngurumo, Njoo! uone.