Revelation 6:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, wafalme wa duniani, wakuu, majemadari, matajiri, wenye nguvu, kila mtumwa na mtu huru, wakajificha mapangoni na kwenye miamba milimani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo wafalme wa dunia, wakuu wote, majemadari, matajiri, wenye nguvu na kila mtu, mtumwa na mtu huru, wakajificha katika mapango na kwenye miamba ya milima.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha watu wote wa ulimwengu, wafalme, watawala, makamanda wa majeshi, matajiri, wenye mamlaka na nguvu, kila mtumwa na asiye mtumwa, walijificha katika mapango na nyuma ya miamba milimani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha wafalme wa duniani, wakuu, majemadari, matajiri, wenye nguvu, kila mtumwa na mtu huru, wakajificha mapangoni na kwenye majabali milimani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, wafalme wa duniani, wakuu, majemadari, matajiri, wenye nguvu, kila mtumwa na mtu huru, wakajificha mapangoni na kwenye miamba milimani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo wafalme wa dunia, wakuu wote, majemadari, matajiri, wenye nguvu na kila mtu, mtumwa na mtu huru, wakajificha katika mapango na kwenye miamba ya milima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo wafalme wa dunia, wakuu wote, majemadari, matajiri, wenye nguvu na kila mtu, mtumwa na mtu huru, wakajificha katika mapango na kwenye miamba ya milima.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na muungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, wafalme wa duniani, wakuu, majemadari, matajiri, wenye nguvu, kila mtumwa na mtu huru, wakajificha mapangoni na kwenye miamba milimani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, wafalme wa nchini, nao walio wakubwa, nao wakuu wa vikosi, nao wenye mali, nao wenye nguvu, nao watumwa wote, nao waungwana wote walipojificha mapangoni na miambani penye milima
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wafalme wa dunia, wakubwa, wakubwa wa waaskari, watajiri, wenye uwezo, na watu wengine wote, watumwa au wenye kuwa huru wakajificha katika mapango na katikati ya mawe ya milima.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na wafalme wa dunia, na wakuu, na matajiri, na majemadari, na wenye nguvu, na killa mtumwa, na mungwana, wakajificha katika pango za chini ya miamba ya milima,