Revelation 6:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakaiambia hiyo milima na hayo majabali, “Tuangukieni, mkatufiche mbali na yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na mbali na ghadhabu ya Mwanakondoo!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakaiita milima na miamba wakisema, “Tuangukieni, mkatufiche na uso wake yeye aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi, na mkatuepushe na ghadhabu ya Mwana-Kondoo!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Waliiambia milima na miamba, “Tuangukieni. Tuficheni mbali na uso wa yule aketiye kwenye kiti cha enzi. Tuficheni dhidi ya hasira ya Mwanakondoo!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakaiambia hiyo milima na hayo majabali, “Tuangukieni, mkatufiche mbali na yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na mbali na ghadhabu ya Mwanakondoo!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakaiambia hiyo milima na hayo majabali, “Tuangukieni, mkatufiche mbali na yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na mbali na ghadhabu ya Mwanakondoo!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakaiita milima na miamba wakisema, “Tuangukieni, mkatufiche na uso wake yeye aketiye kwenye kiti cha enzi na mkatuepushe na ghadhabu ya Mwana-Kondoo!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakaiita milima na miamba wakisema, “Tuangukieni, mkatufiche na uso wake yeye aketiye kwenye kiti cha enzi, na mkatuepushe na ghadhabu ya Mwana-Kondoo!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na kwenye hasira ya Mwana-kondoo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakaiambia hiyo milima na hayo majabali, “Tuangukieni, mkatufiche mbali na yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na mbali na ghadhabu ya Mwanakondoo!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wakiiambia milima na miamba: Tuangukieni, mtufiche machoni pake yeye anayekaa kitini mwa kifalme napo penye makali ya Mwana kondoo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao wakaiambia milima na mawe: “Mutuangukie na kutufunika mbali na yule anayeikaa juu ya kiti cha kifalme na mbali na kasirani ya Mwana-Kondoo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wakaiambia milima na miamba, Tuangukieni, katusetirini, tusione uso wake aketiye juu ya kiti cha enzi wala hasira ya Mwana Kondoo.