Revelation 6:2 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi nikatazama, na kumbe palikuwa na farasi mmoja mweupe hapo. Na mpandafarasi wake alikuwa na upinde, akapewa na taji. Basi, akatoka kama mshindi, aendelee kushinda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nikatazama, na hapo mbele yangu palikuwa na farasi mweupe! Yeye aliyempanda alikuwa na upinde, naye akapewa taji, akampanda akatoka akiwa kama mshindi aelekeaye katika kushinda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, ali akishinda tena apate kushinda.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nilipotazama nilimwona farasi mweupe mbele yangu. Mwendesha farasi aliyekuwa amempanda farasi huyo alikuwa na upinde na alipewa taji. Alimwendesha farasi akatoka kwenda kumshinda adui na ili kupata ushindi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mimi nikatazama, na kumbe palikuwa na farasi mmoja mweupe hapo. Na mpanda farasi wake alikuwa na upinde, akapewa na taji. Basi, akatoka kama mshindi aendelee kushinda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi nikatazama, na kumbe palikuwa na farasi mmoja mweupe hapo. Na mpandafarasi wake alikuwa na upinde, akapewa na taji. Basi, akatoka kama mshindi, aendelee kushinda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nikatazama na hapo mbele yangu alikuwepo farasi mweupe! Yeye aliyempanda alikuwa na upinde, naye akapewa taji, akampanda akatoka akishinda, tena apate kushinda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nikatazama, na hapo mbele yangu alikuwepo farasi mweupe! Yeye aliyempanda alikuwa na upinde, naye akapewa taji, akampanda akatoka akiwa kama mshindi aelekeaye katika kushinda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, huku akishinda tena apate kushinda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi nikatazama, na kumbe palikuwa na farasi mmoja mweupe hapo. Na mpandafarasi wake alikuwa na upinde, akapewa na taji. Basi, akatoka kama mshindi, aendelee kushinda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikatazama, nikaona farasi mweupe, naye aliyempanda alikuwa na uta, akapewa kilemba; kisha yeye aliyekuwa mshindaji akatoka, ashinde tena.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, ali akishinda tena apate kushinda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Niliangalia, nami nikaona farasi mumoja mweupe. Na yule aliyepanda juu yake alikuwa na upindi, akapewa taji. Akatoka akiwa mushindaji na mwenye uwezo wa kuendelea kushinda.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana upinde, akapewa taji, akatoka, akishinda na apate kushinda.