Revelation 6:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nami nikatazama na kumbe palikuwapo farasi mwingine hapo, mwekundu. Mpandafarasi wake alikabidhiwa jukumu la kuondoa amani duniani, watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo akatokea farasi mwingine mwekundu sana. Yeye aliyempanda akapewa uwezo wa kuondoa amani duniani na kuwafanya watu wauane. Yeye akapewa upanga mkubwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nilipotazama nilimwona farasi mwekundu akitokea. Aliyekuwa anamwendesha farasi huyu alipewa mamlaka ya kuondoa amani duniani ili watu wauane. Alipewa upanga mkubwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nami nikatazama na kumbe palikuwapo farasi mwingine hapo, mwekundu. Mpanda farasi wake alikabidhiwa jukumu la kuondoa amani duniani, watu wauane, akapewa upanga mkubwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nami nikatazama na kumbe palikuwapo farasi mwingine hapo, mwekundu. Mpandafarasi wake alikabidhiwa jukumu la kuondoa amani duniani, watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo akatokea farasi mwingine wa rangi nyekundu. Yeye aliyempanda akapewa uwezo wa kuondoa amani duniani na kuwafanya watu wauane. Yeye akapewa upanga mkubwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo akatokea farasi mwingine mwekundu sana. Yeye aliyempanda akapewa uwezo wa kuondoa amani duniani na kuwafanya watu wauane. Yeye akapewa upanga mkubwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, na yeye aliyempanda aliruhusiwa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nami nikatazama na kumbe palikuwapo farasi mwingine hapo, mwekundu. Mpandafarasi wake alikabidhiwa jukumu la kuondoa amani duniani, watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Pakatokea farasi mwingine, ni mwekundu sana; aliyempanda akapewa kuuondoa utengemano katika nchi, wapate kuuana wao kwa wao. Naye akapewa upanga mkubwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha kukatokea farasi mwengine mwekundu. Na yule aliyepanda juu yake akapewa uwezo wa kuondoa amani katika dunia, kusudi watu wauane wao kwa wao. Naye akapewa upanga mukubwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akatoka farasi mwingine mwekundu sana, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katikii inchi, watu wauawe, akapewa upanga mkubwa.