Revelation 7:11 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Malaika wote wakasimama kukizunguka kiti cha enzi, wazee na wale viumbe hai wanne. Wakaanguka kifudifudi mbele ya kiti cha enzi, wakamwabudu Mungu,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Malaika wote walikuwa wamesimama kukizunguka kile kiti cha enzi na wale wazee, na wale viumbe wanne wenye uhai. Wakaanguka kifudifudi mbele ya hicho kiti cha enzi na kumwabudu Mungu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na malaika wote walikuwa wakisimama pande zote za kile kiti cha enzi, na za hao wazee, na za wale wenye uhai wanne, nao wakaanguka kifulifuli mbele ya kile kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wazee na wenye uhai wanne walikuwa pale. Malaika wote walikuwa wamesimama kuwazunguka na kukizunguka kiti cha enzi. Malaika wakainamisha nyuso zao, wakasujudu mpaka chini mbele ya kiti cha enzi, wakamwabudu Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Malaika wote wakasimama kukizunguka kiti cha enzi, wazee na vile viumbe hai vinne. Wakaanguka kifudifudi mbele ya kiti cha enzi, wakamwabudu Mungu,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Malaika wote wakasimama kukizunguka kiti cha enzi, wazee na wale viumbe hai wanne. Wakaanguka kifudifudi mbele ya kiti cha enzi, wakamwabudu Mungu,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Malaika wote walikuwa wamesimama kukizunguka kile kiti cha enzi na wale wazee ishirini na wanne na wale viumbe wanne wenye uhai. Wakaanguka kifudifudi mbele ya hicho kiti cha enzi na kumwabudu Mungu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Malaika wote walikuwa wamesimama kukizunguka kile kiti cha enzi na wale wazee ishirini na wanne na wale viumbe wanne wenye uhai. Wakaanguka kifudifudi mbele ya hicho kiti cha enzi na kumwabudu Mungu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na malaika wote walikuwa wakisimama pande zote za kile kiti cha enzi, na za hao wazee, na za wale wenye uhai wanne, nao wakaanguka kifudifudi mbele ya kile kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Malaika wote wakasimama kukizunguka kiti cha enzi, wazee na wale viumbe hai wanne. Wakaanguka kifudifudi mbele ya kiti cha enzi, wakamwabudu Mungu,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, malaika wote waliosimama na kukizunguka kiti cha kifalme na wale wazee na wale nyama wanne, walipoanguka nyusoni pao mbele ya kiti cha kifalme, wakamsujudia Mungu wakisema:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na malaika wote walikuwa wakisimama pande zote za kile kiti cha enzi, na za hao wazee, na za wale wenye uhai wanne, nao wakaanguka kifulifuli mbele ya kile kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na wamalaika wote waliokuwa wakizunguka kile kiti cha kifalme, wazee na vile viumbe vine vya ajabu, wakainama uso mpaka chini mbele ya kiti cha kifalme, nao wakamwabudu Mungu,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na malaika wote wamesimama pande zote za kiti cha enzi na za wazee na za vile viumbe vine vyenye uhayi, wakaanguka kifudifudi mbele ya kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu,