Revelation 7:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nami nikamjibu, “Mheshimiwa, wewe wajua!” Naye akaniambia, “Hawa ni wale waliopita salama katika ule udhalimu mkuu. Waliyaosha mavazi yao katika damu ya Mwanakondoo, yakawa meupe kabisa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nikamjibu, “Bwana, wewe unajua.” Naye akasema, “Hawa ni wale waliotoka katika ile dhiki kuu, nao wamefua mavazi yao katika damu ya Mwana-Kondoo na kuyafanya meupe kabisa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nikajibu, “Wewe unajua ni akina nani, bwana.” Mzee akasema, “Hawa ni wale waliokuja kutokana na mateso makuu. Wamefua kanzu zao kwa kutumia damu ya Mwanakondoo, wako safi na ni weupe.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nami nikamjibu, “Mheshimiwa, wewe wajua!” Naye akaniambia, “Hawa ni wale waliopita salama katika ule udhalimu mkuu. Waliyaosha mavazi yao katika damu ya Mwanakondoo, yakawa meupe kabisa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nami nikamjibu, “Mheshimiwa, wewe wajua!” Naye akaniambia, “Hawa ni wale waliopita salama katika ule udhalimu mkuu. Waliyaosha mavazi yao katika damu ya Mwanakondoo, yakawa meupe kabisa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nikamjibu, “Bwana, wewe wajua.” Naye akasema, “Hawa ni wale waliotoka katika ile dhiki kuu, nao wamefua mavazi yao katika damu ya Mwana-Kondoo na kuyafanya meupe kabisa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nikamjibu, “Bwana, wewe wajua.” Naye akasema, “Hawa ni wale waliotoka katika ile dhiki kuu, nao wamefua mavazi yao katika damu ya Mwana-Kondoo na kuyafanya meupe kabisa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-kondoo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nami nikamjibu, “Mheshimiwa, wewe wajua!” Naye akaniambia, “Hawa ni wale waliopita salama katika ule udhalimu mkuu. Waliyaosha mavazi yao katika damu ya Mwanakondoo, yakawa meupe kabisa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikamwambia: Bwana wangu, wewe unajua. Akaniambia: Hawa ndio waliotoka katika maumivu makubwa, ndio waliozifua nguo zao na kuzing'aza kwa damu ya Mwana kondoo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nami nikamujibu: “Bwana wangu wewe ndiwe unayejua.” Naye akaniambia: “Hawa ndio wanaotoka katika mateso makubwa. Wamesafisha kanzu zao na kuzifanya kuwa nyeupe katika damu ya Mwana-Kondoo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hawo ndio wanaotoka katika shidda ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao wakayafanya meupe katika damu ya Mwana Kondoo.