Revelation 7:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kabila la Yuda, watu 12,000; kabila la Reubeni, 12,000; kabila la Gadi, 12,000;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kutoka kabila la Yuda elfu kumi na mbili walitiwa muhuri, kutoka kabila la Reubeni elfu kumi na mbili, kutoka kabila la Gadi elfu kumi na mbili,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wa kabila ya Yuda kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri. Wa kabila ya Reubeni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Gadi kumi na mbili elfu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kutoka katika kabila la Yuda walikuwa elfu kumi na mbili Kutoka katika kabila la Rubeni walikuwa elfu kumi na mbili Kutoka katika kabila la Gadi walikuwa elfu kumi na mbili
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kabila la Yuda walikuwa watu kumi na mbili elfu; kabila la Reubeni, kumi na mbili elfu, kabila la Gadi, kumi na mbili elfu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kabila la Yuda, watu 12,000; kabila la Reubeni, 12,000; kabila la Gadi, 12,000;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kutoka kabila la Yuda 12,000, kabila la Reubeni 12,000, kabila la Gadi 12,000,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kutoka kabila la Yuda 12,000 walitiwa muhuri, kutoka kabila la Reubeni 12,000, kutoka kabila la Gadi 12,000,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wa kabila la Yuda elfu kumi na mbili waliotiwa mhuri. Wa kabila la Reubeni elfu kumi na mbili. Wa kabila la Gadi elfu kumi na mbili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kabila la Yuda, watu 12,000; kabila la Reubeni, 12,000; kabila la Gadi, 12,000;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waliotiwa muhuri ya shina la Yuda walikuwa 12000, muhuri ya shina la Rubeni walikuwa 12000, muhuri ya shina la Gadi walikuwa 12000,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wa kabila ya Yuda kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri. Wa kabila ya Reubeni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Gadi kumi na mbili elfu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulikuwa watu elfu kumi na mbili waliopigwa chapa ya muhuri toka kila moja la makabila haya: kabila la Yuda, la Rubeni, la Gadi, la Aseri, la Nafutali, la Manase, la Simeoni, la Lawi, la Isakari, la Zebuluni, la Yosefu na la Benjamina.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wa kabila ya Yuda thenashara elfu waliotiwra muhuri. Wa kabila ya Reuben thenashara elfu. Wa kabila ya Gad thenashara elfu. Wa kablia ya Asher thenashara elfu.