Revelation 8:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
(Nyota hiyo inaitwa “Uchungu.”) Basi, theluthi moja ya maji yakawa machungu; watu wengi wakafa kutokana na maji hayo, kwa sababu yaligeuka kuwa machungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nyota hiyo inaitwa Pakanga. Theluthi ya maji yakawa machungu na watu wengi wakafa kutokana na maji hayo kwa maana yalikuwa machungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na jina lake ile nyota yaitwa Pakanga; theluthi ya maji ikawa pakanga, na wanadamu wengi wakafa kwa maji hayo, kwa kuwa yalitiwa uchungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Jina la nyota hiyo lilikuwa Uchungu. Na theluthi moja ya maji yote yakawa machungu. Watu wengi wakafa kutokana na kunywa maji haya machungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
(Nyota hiyo inaitwa “Uchungu.”) Basi, theluthi moja ya maji yakawa machungu; watu wengi wakafa kutokana na maji hayo, kwa sababu yaligeuka kuwa machungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
(Nyota hiyo inaitwa “Uchungu.”) Basi, theluthi moja ya maji yakawa machungu; watu wengi wakafa kutokana na maji hayo, kwa sababu yaligeuka kuwa machungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nyota hiyo inaitwa Uchungu. Theluthi ya maji yakawa machungu na watu wengi wakafa kutokana na maji hayo kwa maana yalikuwa machungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nyota hiyo inaitwa Uchungu. Theluthi ya maji yakawa machungu na watu wengi wakafa kutokana na maji hayo kwa maana yalikuwa machungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na jina lake ile nyota yaitwa Pakanga; theluthi ya maji ikawa pakanga, na wanadamu wengi wakafa kwa maji hayo, kwa kuwa yalifanywa kuwa machungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
(Nyota hiyo inaitwa “Uchungu.”) Basi, theluthi moja ya maji yakawa machungu; watu wengi wakafa kutokana na maji hayo, kwa sababu yaligeuka kuwa machungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nyota hiyo jina lake huitwa Abisinto. Ndipo, fungu la tatu la maji lilipokuwa na uchungu sana. Watu wengi wakafa kwa yale maji, kwa sababu yalikuwa yenye uchungu uuao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na jina lake ile nyota yaitwa Pakanga; theluthi ya maji ikawa pakanga, na wanadamu wengi wakafa kwa maji hayo, kwa kuwa yalitiwa uchungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
(Jina la ile nyota ni Uchungu.) Basi sehemu moja ya tatu ya maji ikakuwa uchungu, na watu wengi waliokunywa maji yale walikufa kwa sababu ya sumu iliyokuwa ndani yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na jina lake, ile nyota yaitwa Absintho, thuluth ya maji ikawa absintho, na wana Adamu wengi wakafa kwa maji hayo kwa kuwa yalitiwa uchungu.