Revelation 8:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Malaika mwingine akafika, anachukua chetezo cha dhahabu, akasimama mbele ya madhabahu ya kufukizia ubani. Naye akapewa ubani mwingi autoe sadaka pamoja na sala za watu wote wa Mungu juu ya madhabahu ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Malaika mwingine, aliyekuwa na chetezo cha dhahabu, akaja na kusimama mbele ya madhabahu. Akapewa uvumba mwingi ili autoe pamoja na maombi ya watakatifu wote, juu ya yale madhabahu ya dhahabu yaliyo mbele ya kile kiti cha enzi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Malaika mwingine akaja na kusimama kwenye madhabahu. Malaika huyu alikuwa na chetezo ya dhahabu. Malaika alipewa ubani mwingi ili autoe pamoja na maombi ya watakatifu wote wa Mungu. Malaika akaweka sadaka hii juu ya madhabahu ya dhahabu mbele ya kiti cha enzi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Malaika mwingine akafika, akiwa anachukua chetezo cha dhahabu, akasimama mbele ya madhabahu ya kufukizia ubani. Naye akapewa ubani mwingi autoe sadaka pamoja na sala za watu wote wa Mungu, juu ya madhabahu ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Malaika mwingine akafika, anachukua chetezo cha dhahabu, akasimama mbele ya madhabahu ya kufukizia ubani. Naye akapewa ubani mwingi autoe sadaka pamoja na sala za watu wote wa Mungu juu ya madhabahu ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Malaika mwingine aliyekuwa na chetezo cha dhahabu, akaja na kusimama mbele ya madhabahu. Akapewa uvumba mwingi ili autoe pamoja na maombi ya Watakatifu wote, juu ya ile madhabahu ya dhahabu iliyoko mbele ya kile kiti cha enzi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Malaika mwingine aliyekuwa na chetezo cha dhahabu, akaja na kusimama mbele ya madhabahu. Akapewa uvumba mwingi ili autoe pamoja na maombi ya watakatifu wote, juu ya yale madhabahu ya dhahabu yaliyo mbele ya kile kiti cha enzi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, akiwa na chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Malaika mwingine akafika, anachukua chetezo cha dhahabu, akasimama mbele ya madhabahu ya kufukizia ubani. Naye akapewa ubani mwingi autoe sadaka pamoja na sala za watu wote wa Mungu juu ya madhabahu ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akaja malaika mwingine, akasimama mbele ya meza ya Bwana; huyu alikuwa na chetezo cha dhahabu cha kuvukizia. Akapewa uvumba mwingi, auvukize juu ya meza ya Bwana iliyo ya dhahabu, iliyoko mbele ya kiti cha kifalme, watakatifu wote watakapoomba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha malaika mwingine akakuja kusimama karibu na mazabahu. Alikuwa akishika chetezo cha zahabu. Naye akapewa ubani mwingi kusudi autoe sadaka pamoja na maombi ya watu wote wa Mungu juu ya mazabahu ya zahabu iliyokuwa mbele ya kiti cha kifalme.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhbahu, mwenye cheteso cha dhahabu, akapewa manukato mengi illi ayatie pamoja na sala za watakatifu juu ya madhbahu ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi.