Revelation 8:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
theluthi moja ya viumbe vya baharini vikafa, na theluthi moja ya meli zikaharibiwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
theluthi ya viumbe vyenye uhai vilivyoishi baharini vikafa, na theluthi ya meli zikaharibiwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakafa theluthi ya viumbe vilivyomo baharini, vyenye uhai; theluthi ya merikebu zikaharibiwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na theluthi moja ya viumbe walioumbwa wanaokaa baharini wakafa na ya meli theluthi moja zikaharibika.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
theluthi moja ya viumbe vya baharini vikafa na theluthi moja ya meli zikaharibiwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
theluthi moja ya viumbe vya baharini vikafa, na theluthi moja ya meli zikaharibiwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
theluthi ya viumbe vyenye uhai viishivyo baharini vikafa na theluthi ya meli zikaharibiwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
theluthi ya viumbe vyenye uhai viishivyo baharini vikafa na theluthi ya meli zikaharibiwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakafa theluthi ya viumbe vilivyomo baharini, vyenye uhai; theluthi ya meli zikaharibiwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
theluthi moja ya viumbe vya baharini vikafa, na theluthi moja ya meli zikaharibiwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
hata fungu la tatu la viumbe vya baharini vilivyokuwa vyenye uzima vikafa, hata fungu la tatu la vyombo vikaangamia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakafa theluthi ya viumbe vilivyomo baharini, vyenye uhai; theluthi ya merikebu zikaharibiwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sehemu moja ya tatu ya viumbe vinavyoishi katika bahari vikakufa, na sehemu moja ya tatu ya mashua ikaharibika.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakafa thuluth ya viumbe vilivyo katika bahari, vyenye uhayi: thuluth ya merikebu zikaharibiwa.