Revelation 9:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walikuwa na mikia na miiba kama nge, na kwa mikia hiyo, walikuwa na nguvu ya kuwadhuru watu kwa muda wa miezi mitano.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walikuwa na mikia yenye miiba ya kuumia, kama nge. Nguvu yao ya kutesa watu kwa huo muda wa miezi mitano ilikuwa katika mikia yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wana mikia kama ya nge, na miiba; na nguvu yao ya kuwadhuru wanadamu miezi mitano ilikuwa katika mikia yao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Walikuwa na mikia kama ya nge. Nguvu ya kuwasababishia wanadamu maumivu kwa miezi mitano ilikuwa kwenye mikia yao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walikuwa na mikia na miiba kama ng'e, na kwa mikia hiyo, walikuwa na nguvu ya kuwadhuru watu kwa muda wa miezi mitano.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walikuwa na mikia na miiba kama nge, na kwa mikia hiyo, walikuwa na nguvu ya kuwadhuru watu kwa muda wa miezi mitano.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walikuwa na mikia yenye miiba ya kuumia kama nge. Nguvu yao ya kutesa watu kwa huo muda wa miezi mitano ilikuwa katika hiyo mikia yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walikuwa na mikia yenye miiba ya kuumia kama nge. Nguvu yao ya kutesa watu kwa huo muda wa miezi mitano ilikuwa katika hiyo mikia yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wana mikia kama ya nge, na miiba; na nguvu yao ya kuwadhuru wanadamu miezi mitano ilikuwa katika mikia yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walikuwa na mikia na miiba kama nge, na kwa mikia hiyo, walikuwa na nguvu ya kuwadhuru watu kwa muda wa miezi mitano.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walikuwa wenye mikia kama ya nge yenye machomeo; namo mikiani mwao ndimo, nguvu zao zilimokuwa za kuwapotoa watu miezi mitano.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wana mikia kama ya nge, na miiba; na nguvu yao ya kuwadhuru wanadamu miezi mitano ilikuwa katika mikia yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walikuwa na mikia kama ya nge na yenye kuchoma kama miiba. Uwezo wao wa kuwatesa watu kwa muda wa ile miezi mitano ulikuwa ndani ya mikia yao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na wana mikia kama ya nge, na palikuwa kama viumo katika mikia yao. Na nguvu yao kuwadhuru wana Adamu miezi mitano.