Revelation 9:17 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivi ndivyo nilivyowaona hao farasi na wapandafarasi katika hiyo njozi: Walikuwa na ngao vifuani zilizokuwa moto mtupu, zenye rangi ya samawati na manjano kama madini ya kiberiti. Vichwa vya hao farasi vilikuwa kama vya simba; na moto, moshi, na madini ya kiberiti vilikuwa vinatoka vinywani mwao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivi ndivyo nilivyowaona hao farasi na wapanda farasi katika maono yangu: Wapanda farasi walivaa dirii vifuani zenye rangi nyekundu sana kama ya moto, na yakuti samawi, na kiberiti. Vichwa vya hao farasi vilikuwa kama vichwa vya simba, na moto, moshi na kiberiti vilitoka vinywani mwao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hiyo ndivyo nilivyowaona hao farasi katika maono yangu, nao waliokaa juu yao, wana dirii kifuani, kama za moto, na za samawi, na za kiberiti; na vichwa vya farasi hao ni kama vichwa vya simba, na katika vinywa vyao hutoka moto na moshi na kiberiti.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Katika maono yangu, niliona farasi na waendesha farasi wakiwa juu ya farasi. Walionekana hivi: Walivaa dirii za chuma vifuani mwao zilizokuwa za rangi nyekundu, rangi ya bahari iliyoiva na za rangi ya njano kama baruti. Vichwa vya farasi vilionekana kama vichwa vya simba. Farasi walikuwa wanatoa moto, moshi na baruti katika vinywa vyao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hivi ndivyo nilivyowaona hao farasi na wapanda farasi katika hiyo njozi: Walikuwa na ngao vifuani zilizokuwa moto mtupu, zenye rangi ya samawati na njano kama kiberiti. Vichwa vya hao farasi vilikuwa kama vya simba; na moto, moshi, na kiberiti vilikuwa vinatoka kinywani mwao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivi ndivyo nilivyowaona hao farasi na wapandafarasi katika hiyo njozi: Walikuwa na ngao vifuani zilizokuwa moto mtupu, zenye rangi ya samawati na manjano kama madini ya kiberiti. Vichwa vya hao farasi vilikuwa kama vya simba; na moto, moshi, na madini ya kiberiti vilikuwa vinatoka vinywani mwao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivi ndivyo nilivyowaona hao farasi na wapanda farasi katika maono yangu: Wapanda farasi walivaa dirii vifuani zenye rangi ya moto na yakuti samawi na kiberiti. Vichwa vya hao farasi vilikuwa kama vichwa vya simba. Moto, moshi na kiberiti vilitoka vinywani mwao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivi ndivyo nilivyowaona hao farasi na wapanda farasi katika maono yangu: Wapanda farasi walivaa dirii vifuani zenye rangi nyekundu sana kama ya moto na yakuti samawi na kiberiti. Vichwa vya hao farasi vilikuwa kama vichwa vya simba, na moto, moshi na kiberiti vilitoka vinywani mwao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hivyo ndivyo nilivyowaona hao farasi katika maono yangu, nao waliokaa juu yao, wana dirii kifuani, za wekundu kama wa moto, na buluu kama johari ya rangi ya samawati na manjano kama kiberiti, na vichwa vya farasi hao ni kama vichwa vya simba, na katika vinywa vyao hutoka moto na moshi na kiberiti.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivi ndivyo nilivyowaona hao farasi na wapandafarasi katika hiyo njozi: Walikuwa na ngao vifuani zilizokuwa moto mtupu, zenye rangi ya samawati na manjano kama madini ya kiberiti. Vichwa vya hao farasi vilikuwa kama vya simba; na moto, moshi, na madini ya kiberiti vilikuwa vinatoka vinywani mwao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nilipowatazama wale farasi nao waliowapanda, nikawaona kuwa hivyo: walikuwa wamevaa nguo za vyuma kama za moto, nyingine nyeusi, nyingine za manjano. Vichwa vya farasi vilikuwa kama vya simba, tena katika vinywa vyao hutoka moto na moshi na viberitiberiti.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hiyo ndivyo nilivyowaona hao farasi katika maono yangu, nao waliokaa juu yao, wana dirii kifuani, kama za moto, na za samawi, na za kiberiti; na vichwa vya farasi hao ni kama vichwa vya simba, na katika vinywa vyao hutoka moto na moshi na kiberiti.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na katika maono yale, nikaona wale farasi pamoja na wale waaskari waliopanda juu yao. Waaskari wale walikuwa na ngao zenye rangi nyekundu kama moto na zingine za rangi ya samawi na ya kimanjano kama kiberiti. Vichwa vya farasi wale vilikuwa kama vichwa vya simba, na ndani ya vinywa vyao mulitoka moto, moshi na mawe ya viberiti.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ndivyo nilivyowaona farasi katika maono yangu, nao waliokaa juu yao, wana mabamba kifuani, ya moto, na ya samawati, na ya kiberiti; na vichwa vya farasi hawo kama vichwa vya simba, kukatoka katika vinywa vyao moto na moshi na kiberiti.