Revelation 9:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Theluthi moja ya wanadamu waliuawa kwa mabaa hayo matatu, yaani moto, moshi na madini ya kiberiti, yaliyokuwa yanatoka katika vinywa vyao;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa mapigo hayo matatu, yaani huo moto, moshi na kiberiti, vilivyotoka kwenye vinywa vya hao farasi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa mapigo matatu hayo, kwa moto huo na moshi huo na kiberiti hicho, yaliyotoka katika vinywa vyao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Theluthi ya watu wote duniani walikufa kutokana na mapigo haya matatu yaliyokuwa yanatoka vinywani mwa farasi: moto, moshi na baruti.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Theluthi moja ya wanaadamu waliuawa kwa mabaa hayo matatu yaani, moto, moshi na kiberiti, yaliyokuwa yanatoka katika vinywa vyao;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Theluthi moja ya wanadamu waliuawa kwa mabaa hayo matatu, yaani moto, moshi na madini ya kiberiti, yaliyokuwa yanatoka katika vinywa vyao;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa maafa hayo matatu, yaani, huo moto, moshi na kiberiti, vilivyotoka kwenye vinywa vya hao farasi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa mapigo hayo matatu, yaani, huo moto, moshi na kiberiti, vilivyotoka kwenye vinywa vya hao farasi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa mapigo matatu hayo, kwa moto huo na moshi huo na kiberiti hicho, yaliyotoka katika vinywa vyao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Theluthi moja ya wanadamu waliuawa kwa mabaa hayo matatu, yaani moto, moshi na madini ya kiberiti, yaliyokuwa yanatoka katika vinywa vyao;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Fungu la tatu la watu likauawa kwa mapigo hayo matatu, kwa moto na kwa moshi na kwa viberitiberiti vilivyotoka vinywani mwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa mapigo matatu hayo, kwa moto huo na moshi huo na kiberiti hicho, yaliyotoka katika vinywa vyao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na sehemu moja ya tatu ya wanadamu wakauawa kwa mapigo hayo matatu: kwa moto, moshi na viberiti vilivyotoka ndani ya vinywa vya wale farasi,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Thuluth ya wana Adamu wakauawa kwa matatu bayo, kwa moto huo na moshi huo na kiberiti hicho kilichotoka katika vinywa vyao.