Revelation 9:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, nyota hiyo ikafungua shimo la kuzimu, kukatoka moshi wa tanuri kubwa. Jua na anga vikatiwa giza kwa moshi huo wa kuzimu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipolifungua hilo Shimo, moshi ukapanda kutoka humo kama moshi wa tanuru kubwa sana. Jua na anga vikatiwa giza na ule moshi uliotoka katika hilo Shimo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha nyota ikafungua shimo refu sana liendalo kuzimu. Moshi ukatoka kwenye shimo kama moto utokao kwenye tanuru kubwa. Jua na anga vikawa giza kwa sababu ya moshi uliotoka kwenye shimo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, nyota hiyo ikafungua shimo la Kuzimu, kukatoka moshi wa tanuru kubwa. Jua na anga vikatiwa giza kwa moshi huo wa Kuzimu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, nyota hiyo ikafungua shimo la kuzimu, kukatoka moshi wa tanuri kubwa. Jua na anga vikatiwa giza kwa moshi huo wa kuzimu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipolifungua hilo Shimo lisilo na mwisho, moshi ukapanda kutoka humo kama moshi wa tanuru kubwa sana. Jua na anga vikatiwa giza na ule moshi uliotoka katika hilo shimo lisilokuwa na mwisho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipolifungua hilo Shimo, moshi ukapanda kutoka humo kama moshi wa tanuru kubwa sana. Jua na anga vikatiwa giza na ule moshi uliotoka katika hilo Shimo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuri kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, nyota hiyo ikafungua shimo la kuzimu, kukatoka moshi wa tanuri kubwa. Jua na anga vikatiwa giza kwa moshi huo wa kuzimu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ikakifungua hicho kisima cha kuzimu. Ndipo, ulipopanda moshi kutoka mle kisimani kama moshi wa jiko kubwa. Jua likatiwa giza, hata anga vilevile kwa ajili ya moshi huo wa kisimani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyota ile ikafungua hilo shimo. Moshi unaokuwa kama moshi wa furu kubwa ukapanda toka ndani ya shimo lile. Giza la ule moshi uliotoka ndani ya lile shimo ulifunika jua na anga.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akalifungua shimo la abuso; moshi ukapanda kutoka lile shimo kama moshi wa tanuru kubwa: juu na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimo.