Revelation 9:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa kuonekana, nzige hao walikuwa kama farasi waliowekwa tayari kwa vita. Juu ya vichwa vyao walikuwa na taji zilizo kama za dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama za binadamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale nzige walikuwa na umbo kama la farasi waliotayarishwa kwa ajili ya vita. Kwenye vichwa vyao kulikuwa na kitu kama taji za dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama za binadamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na maumbo ya hao nzige yalikuwa kama farasi waliowekwa tayari kwa vita, na juu ya vichwa vyao kama taji, mfano wa dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama nyuso za wanadamu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nzige hao walionekana kama farasi walioandaliwa kwa ajili ya mapigano. Vichwani mwao walivaa kitu kilichoonekana kama taji ya dhahabu. Nyuso zao zilionekana kama nyuso za wanadamu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa kuonekana, nzige hao walikuwa kama farasi waliowekwa tayari kwa vita. Juu ya vichwa vyao walikuwa na taji zilizo kama za dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama za binadamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa kuonekana, nzige hao walikuwa kama farasi waliowekwa tayari kwa vita. Juu ya vichwa vyao walikuwa na taji zilizo kama za dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama za binadamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale nzige walikuwa na umbo kama la farasi waliotayarishwa kwa ajili ya vita. Kwenye vichwa vyao kulikuwa na kitu kama taji za dhahabu na nyuso zao zilikuwa kama za binadamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale nzige walikuwa na umbo kama la farasi waliotayarishwa kwa ajili ya vita. Kwenye vichwa vyao kulikuwa na kitu kama taji za dhahabu na nyuso zao zilikuwa kama za binadamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na maumbo ya hao nzige yalikuwa kama farasi waliowekwa tayari kwa vita, na juu ya vichwa vyao kama mataji, mfano wa dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama nyuso za wanadamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa kuonekana, nzige hao walikuwa kama farasi waliowekwa tayari kwa vita. Juu ya vichwa vyao walikuwa na taji zilizo kama za dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama za binadamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Umbo la nzige hao lilikuwa limefanana kama la farasi walio tayari kupiga vita. Vichwani pao hapo juu palikuwa kama vilemba vilivyofanana na dhahabu. Nyuso zao lilikuwa kama nyuso za watu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na maumbo ya hao nzige yalikuwa kama farasi waliowekwa tayari kwa vita, na juu ya vichwa vyao kama taji, mfano wa dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama nyuso za wanadamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Umbo la nzige wale lilifanana na farasi waliopambwa kwa kupigana vita. Juu ya vichwa vyao kulikuwa vitu vinavyofanana na taji za zahabu, na nyuso zao zilifanana kama nyuso za watu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na maumbo ya zile nzige kama farasi waliowekwa tayari kwa vita, na juu ya vichwa vyao kama taji, mfano wa dhahabu, na nyuso zao kama nyuso za wana Adamu.