Romans 1:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sioni aibu kutangaza Habari Njema; yenyewe ni nguvu ya Mungu inayowaokoa wote wanaoamini: Wayahudi kwanza na wasio Wayahudi pia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mimi siionei haya Injili, kwa maana ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye, kwanza kwa Myahudi na kwa Myunani pia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa mimi hakuna haya katika kuhubiri Habari Njema. Ninayo furaha kwa sababu Habari Njema ni nguvu ya Mungu inayomwokoa kila anayeamini, yaani inawaokoa Wayahudi kwanza, na sasa inawaokoa Mataifa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sioni aibu kutangaza Habari Njema; yenyewe ni nguvu ya Mungu inayowaokoa wote wanaoamini: Wayahudi kwanza, na wasio Wayahudi pia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sioni aibu kutangaza Habari Njema; yenyewe ni nguvu ya Mungu inayowaokoa wote wanaoamini: Wayahudi kwanza na wasio Wayahudi pia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mimi siionei haya Injili ya Kristo kwa maana ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye, kwanza kwa Myahudi na kwa Myunani pia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mimi siionei haya Injili ya Al-Masihi kwa maana ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye, kwanza kwa Myahudi na kwa Myunani pia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Mgiriki pia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sioni aibu kutangaza Habari Njema; yenyewe ni nguvu ya Mungu inayowaokoa wote wanaoamini: Wayahudi kwanza na wasio Wayahudi pia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maana sioni soni ya kuutangaza Utume mwema wa Kristo, kwani unayo nguvu ya Mungu ya kuwaokoa wo wote wanaoutegemea, kwanza Wayuda, kisha Wagriki nao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi sisikii haya juu ya Habari Njema, kwa sababu huo ndio uwezo wa Mungu unaowaokoa wote wanaoamini, kwanza Wayuda na kisha watu wa mataifa mengine vilevile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kwa maana siionci haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokofu, kwa killa aaminiye, kwa Myahudi kwanza, hatta kwa Myunani pia.