Romans 1:28 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa vile watu walikataa kumtambua Mungu, Mungu amewaacha katika fikira zao potovu, wakafanya yale ambayo hawangestahili kufanya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nao kwa kuwa hawakuona umuhimu wa kudumisha ufahamu wa Mungu, yeye akawaachilia wafuate akili za upotovu, watende mambo yale yasiyostahili kutendwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu hawa waliona kuwa haikuwa muhimu kwao kumkubali Mungu katika fikra zao. Hivyo Mungu akawaacha wayafuate mawazo yao mabaya. Hivyo hufanya mambo ambayo mtu yeyote hapaswi kufanya.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa vile watu walikataa kumtambua Mungu, Mungu amewaacha katika fikira zao potovu, wakafanya yale ambayo hawangestahili kufanya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa vile watu walikataa kumtambua Mungu, Mungu amewaacha katika fikira zao potovu, wakafanya yale ambayo hawangestahili kufanya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nao kwa kuwa walikataa kumkubali Mungu, yeye akawaacha wafuate akili zao za upotovu, watende mambo yale yasiyostahili kutendwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nao kwa kuwa hawakuona umuhimu wa kudumisha ufahamu wa Mungu, yeye akawaachilia wafuate akili za upotovu, watende mambo yale yasiyostahili kutendwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa vile watu walikataa kumtambua Mungu, Mungu amewaacha katika fikira zao potovu, wakafanya yale ambayo hawangestahili kufanya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena kwa hivyo, walivyokataa kumshika Mungu na kumtambua, Mungu aliwatupa, wafuate mawazo ya ujinga na kufanya yasiyompasa mtu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivi kufuatana na vile walivyokataa kumutambua Mungu, Mungu akawaacha wafuate akili yao ya upotevu, kusudi wafanye mambo wasiyopaswa kufanya.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wuyafanye yasiyowapasa;