Romans 10:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jambo hili ni kwa wote, kwani hakuna tofauti kati ya Wayahudi na wasio Wayahudi; Bwana wa wote ni mmoja, naye ni mkarimu sana kwao wote wamwombao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana hakuna tofauti kati ya Myahudi na mtu wa Mataifa, yeye ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yanasema hivi kwa sababu hakuna tofauti kati ya Wayahudi na wasio Wayahudi. Bwana yule yule ndiye Bwana wa watu wote. Naye humbariki sana kila amwombaye akitaka msaada.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Jambo hili ni kwa wote, kwani hakuna tofauti kati ya Wayahudi na wasio Wayahudi; Bwana wa wote ni mmoja, naye ni mkarimu sana kwao wote wamwombao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jambo hili ni kwa wote, kwani hakuna tofauti kati ya Wayahudi na wasio Wayahudi; Bwana wa wote ni mmoja, naye ni mkarimu sana kwao wote wamwombao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana hakuna tofauti kati ya Myahudi na Myunani, yeye ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana hakuna tofauti kati ya Myahudi na Myunani, yeye ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Mgiriki; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye ukarimu mwingi kwa wote wamwitao;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jambo hili ni kwa wote, kwani hakuna tofauti kati ya Wayahudi na wasio Wayahudi; Bwana wa wote ni mmoja, naye ni mkarimu sana kwao wote wamwombao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hapa hawachaguliwi Wayuda na Wagriki; kwani aliye Bwana wao wote ni yuyu huyu mmoja, ni mwenye magawio yanayowatoshea wote wanaomtambikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi hakuna tofauti kati ya Wayuda na watu wa mataifa mengine, kwa maana Bwana wa wote ni mumoja tu, na anawabariki sana wote wanaomusihi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana hapana tofanti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri wa kufaa watu wote wamwitiao;