Romans 10:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini nauliza: Je, hawakuusikia huo ujumbe? Naam, waliusikia; kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Sauti yao imeenea duniani kote; maneno yao yamefika mpaka kingo za ulimwengu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini nauliza: Je, wao hawakusikia? Naam, wamesikia, kwa maana: “Sauti yao imeenea duniani pote, nayo maneno yao yameenea hadi miisho ya ulimwengu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini nasema, Je! Wao hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao imeenea duniani mwote, Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini nauliza, “Je, watu hao walizisikia Habari Njema?” Ndio Kwa kweli walizisikia kama Maandiko yanavyosema, “Sauti zao zilitoka na kuenea duniani kote. Maneno yao yakaenda kila mahali ulimwenguni.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini nauliza: je, hawakuusikia huo ujumbe? Naam, waliusikia; kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Sauti yao imeenea duniani kote; maneno yao yamefika mpaka kingo za ulimwengu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini nauliza: je, hawakuusikia huo ujumbe? Naam, waliusikia; kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Sauti yao imeenea duniani kote; maneno yao yamefika mpaka kingo za ulimwengu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini nauliza, Je, wao hawakusikia? Naam, wamesikia, kwa maana: “Sauti yao imeenea duniani kote, nayo maneno yao yamefika hadi miisho ya ulimwengu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini nauliza: Je, wao hawakusikia? Naam, wamesikia, kwa maana: “Sauti yao imeenea duniani pote, nayo maneno yao yameenea hadi miisho ya ulimwengu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini nasema, Je! Wao hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao imeenea duniani kote, Na maneno yao hadi katika miisho ya ulimwengu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini nauliza: Je, hawakuusikia huo ujumbe? Naam, waliusikia; kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Sauti yao imeenea duniani kote; maneno yao yamefika mpaka kingo za ulimwengu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini niseme: Hawakusikia? Kusikia wamesikia. Uvumi wao ulitokea katika nchi zote; nayo maneno yao yalifika hata mapeoni kwa ulimwengu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini nasema, Je! Wao hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao imeenea duniani mwote, Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi ninauliza: hawakusikia habari hii? Ndiyo, wameisikia! Kwa maana Maandiko Matakatifu yanasema: “Sauti yao imesikilika katika dunia yote, maneno yao yamefika pande zote za dunia.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini nasema, Wao hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao imetoka ikaenea katika inchi yote, Na maneno yao hatta miisho ya ulimwengu.