Romans 10:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena nauliza: Je, yawezekana kwamba watu wa Israeli hawakufahamu? Mose mwenyewe ni wa kwanza kujibu: “Nitawafanyeni muwaonee wivu watu ambao si taifa; nitawafanyeni muwe na hasira juu ya taifa la watu wapumbavu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nami nauliza tena: Je, Waisraeli hawakuelewa? Kwanza, Musa asema, “Nitawafanya mwe na wivu kwa watu wale ambao si taifa. Nitawakasirisha kwa taifa lile lisilo na ufahamu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini nasema, Je! Waisraeli hawakufahamu? Kwanza Musa anena,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini tena nauliza, “Je, watu wa Israeli hawakuelewa?” Ndiyo, walielewa. Musa alikuwa wa kwanza kujibu swali hili. Na anasema haya kwa ajili ya Mungu: “Nitawatumia wale ambao siyo Taifa halisi ili liwafanye muone wivu. Nitalitumia taifa ambalo halielewi ili mkasirike.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tena nauliza: je, yawezekana kwamba watu wa Israeli hawakufahamu? Mose mwenyewe ni kwa kwanza kujibu: “Nitawafanyeni mwaonee wivu watu ambao si taifa; nitawafanyeni muwe na hasira juu ya taifa la watu wapumbavu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena nauliza: je, yawezekana kwamba watu wa Israeli hawakufahamu? Mose mwenyewe ni wa kwanza kujibu: “Nitawafanyeni muwaonee wivu watu ambao si taifa; nitawafanyeni muwe na hasira juu ya taifa la watu wapumbavu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nami nauliza tena: Je, Waisraeli hawakuelewa? Kwanza, Mose asema, “Nitawafanya mwe na wivu kwa watu wale ambao si taifa. Nitawakasirisha kwa taifa la watu wasio na ufahamu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nami nauliza tena: Je, Waisraeli hawakuelewa? Kwanza, Musa asema, “Nitawafanya mwe na wivu kwa watu wale ambao si taifa. Nitawakasirisha kwa taifa lile lisilo na ufahamu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini nasema, Je! Waisraeli hawakufahamu? Kwanza Musa anena, Nitawatia wivu kwa watu ambao si taifa, Kwa taifa lisilo na fahamu nitawakasirisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena nauliza: Je, yawezekana kwamba watu wa Israeli hawakufahamu? Mose mwenyewe ni wa kwanza kujibu: “Nitawafanyeni muwaonee wivu watu ambao si taifa; nitawafanyeni muwe na hasira juu ya taifa la watu wapumbavu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Au niseme: Waisiraeli hawakulitambua? Kwanza Mose anasema: Mimi na niwachokoze ninyi nikiwaletea watu wasio watu, na niwakasirishe ninyi nikiwaletea taifa la watu wasiojua maana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini nasema, Je! Waisraeli hawakufahamu? Kwanza Musa anena, Nitawatia wivu kwa watu ambao si taifa, Kwa taifa lisilo na fahamu nitawaghadhibisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninauliza tena: Waisraeli hawakufahamu kitu? Kwanza Musa alikuwa amekwisha kujibu: “Nitawafanya kuwa na wivu juu ya watu wasiokuwa taifa. Nitawakasirikisha ninyi kwa njia ya taifa pumbafu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini nasema, Israeli hakufahamu? Hapo kwanza Musa anena, Nitawatieni moyo wa bidii kwa watu wasio taifa, Kwa taifa lisilo na fahamu nitawaghadhabisha.