Romans 10:20 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena Isaya anathubutu hata kusema: “Wale ambao hawakunitafuta wamenipata; nimejionesha kwao wasiouliza habari zangu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye Isaya kwa ujasiri mwingi anasema, “Nimeonekana na watu wale ambao hawakunitafuta. Nilijifunua kwa watu wale ambao hawakunitafuta.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Isaya anao ujasiri mwingi, asema,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha Isaya ana ujasiri wa kutosha kusema haya kwa ajili ya Mungu: “Watu walionipata mimi hawakuwa wakinitafuta. Nilijitambulisha kwa watu ambao hawakuwa wakinitafuta.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tena Isaya anathubutu hata kusema: “Wale ambao hawakunitafuta wamenipata; nimejionyesha kwao wasiouliza habari zangu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena Isaya anathubutu hata kusema: “Wale ambao hawakunitafuta wamenipata; nimejionesha kwao wasiouliza habari zangu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye Isaya kwa ujasiri mwingi anasema, “Watu wale waliokuwa hawanitafuti, wamenipata; nimejidhihirisha kwa watu wale waliokuwa hawaniulizii.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye Isaya kwa ujasiri mwingi anasema, “Nimeonekana na watu wale ambao hawakunitafuta. Nilijifunua kwa watu wale ambao hawakunitafuta.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Isaya anao ujasiri mwingi, asema, Nilipatikana nao wasionitafuta, Nilidhihirika kwao wasioniulizia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena Isaya anathubutu hata kusema: “Wale ambao hawakunitafuta wamenipata; nimejionesha kwao wasiouliza habari zangu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yesaya anajipa moyo wa kusema: Nimeonwa nao wasionitafuta, nikawatokea wasioniuliza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Isaya anao ujasiri mwingi, asema, Nalipatikana nao wasionitafuta, Nalidhihirika kwao wasioniulizia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Isaya kwa uhodari anaongeza kusema maneno haya: “Nimepatikana kwa watu wasionitafuta, nimejifunua kwa watu wasioniuliza.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na Isaya ana ujasiri mwingi, anasema, Nalipatikana nao wasionitafuta, Nalidhihirika kwao wasioniulizia.