Romans 10:21 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kuhusu Israeli anasema: “Mchana kutwa niliwanyoshea mikono yangu watu waasi na wasiotii.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kuhusu Israeli anasema, “Mchana kutwa nimewanyooshea watu wakaidi na wasiotii mikono yangu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini kwa Israeli asema, Mchana kutwa naliwanyoshea mikono watu wasiotii na wakaidi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini kuhusu watu wa Israeli Mungu anasema, “Kutwa nzima nilisimama nikiwa tayari kuwakubali watu hawa, lakini ni wakaidi na wamekataa kunitii.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini kuhusu Israeli anasema: “Mchana kutwa niliwanyoshea mikono yangu watu waasi na wasiotii.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kuhusu Israeli anasema: “Mchana kutwa niliwanyoshea mikono yangu watu waasi na wasiotii.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kuhusu Israeli anasema, “Mchana kutwa nimewanyoshea watu wakaidi na wasiotii mikono yangu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kuhusu Israeli anasema, “Mchana kutwa nimewanyooshea watu wakaidi na wasiotii mikono yangu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini kwa Israeli asema, Mchana kutwa niliwanyoshea mikono watu wasiotii na wakaidi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kuhusu Israeli anasema: “Mchana kutwa niliwanyoshea mikono yangu watu waasi na wasiotii.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Waisiraeli anawaambia: Mchana kutwa naliikunjua mikono yangu, nipungie ukoo wa watu wasioonyeka, walio wabishi tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini kwa Israeli asema, Mchana kutwa naliwanyoshea mikono watu wasiotii na wakaidi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini juu ya Waisraeli anasema hivi: “Muchana kutwa ninanyoosha mikono yangu kwa kuita taifa lenye uasi na ubishi.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini kwa israeli asema, Mchana kutwa naliwanyoshea mikono watu wasiotii na ubishi.