Romans 10:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana kwa kuja kwake Kristo, sheria imefikia kikomo chake, ili wote wanaoamini wafanywe waadilifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana Al-Masihi ni ukomo wa sheria ili kila mtu aaminiye ahesabiwe haki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sheria ilifikia mwisho wake wakati Kristo alipolikamilisha kusudi lake. Sasa kila mtu anayeiweka imani yake kwake anahesabiwa haki mbele za Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana kwa kuja kwake Kristo, Sheria imefikia kikomo chake, ili kila mtu anayeamini akubaliwe kuwa mwadilifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana kwa kuja kwake Kristo, sheria imefikia kikomo chake, ili wote wanaoamini wafanywe waadilifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana Kristo ni ukomo wa sheria ili kuwe na haki kwa kila mtu aaminiye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana Al-Masihi ni ukomo wa sheria ili kuwe na haki kwa kila mtu aaminiye.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana kwa kuja kwake Kristo, sheria imefikia kikomo chake, ili wote wanaoamini wafanywe waadilifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani timilizo la Maonyo ni Kristo, kila mwenye kumtegemea ajipatie wongofu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana kwa njia ya Kristo, Sheria imepata kufikia ukomo wake kusudi kila mutu anayeamini apate kuhesabiwa haki mbele ya Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana Kristo ni mwisho wa sharia, illi killa aaminiye apate haki.