Romans 10:5 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhusu kuwa mwadilifu kwa kuitii sheria, Mose aliandika hivi: “Mtu yeyote anayetimiza matakwa ya sheria ataishi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Musa anaandika kuhusu haki ile itokanayo na sheria, kwamba, “Mtu atendaye matendo hayo ataishi kwa hayo.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana Musa aliandika juu ya haki itokayo kwa sheria, ya kuwa, Mtu afanyaye hiyo ataishi kwa hiyo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Musa anaandika juu ya kuhesabiwa haki kwa kuifuata sheria. Anasema: “Ili kupata uzima katika sheria imempasa mtu kuzitii.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kuhusu kukubaliwa kuwa mwadilifu kwa kuitii Sheria, Mose aliandika hivi: “Mtu yeyote anayetimiza matakwa ya Sheria ataishi.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhusu kuwa mwadilifu kwa kuitii sheria, Mose aliandika hivi: “Mtu yeyote anayetimiza matakwa ya sheria ataishi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mose anaandika kuhusu haki ile itokanayo na sheria, kwamba, “Mtu atendaye mambo hayo ataishi kwa hayo.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Musa anaandika kuhusu haki ile itokanayo na sheria, kwamba, “Mtu atendaye matendo hayo ataishi kwa hayo.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana Musa aliandika juu ya haki itokayo kwa sheria, ya kuwa, Mtu afanyaye hiyo ataishi kwa hiyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhusu kuwa mwadilifu kwa kuitii sheria, Mose aliandika hivi: “Mtu yeyote anayetimiza matakwa ya sheria ataishi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Mose aliandika: Anayeufanya wongofu ulioagizwa na Maonyo mtu huyo atapata uzima kwa njia hiyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana Musa aliandika juu ya haki itokayo kwa sheria, ya kuwa, Mtu afanyaye hiyo ataishi kwa hiyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Haya ndiyo mambo Musa aliyoandika juu ya kuhesabiwa haki mbele ya Mungu kwa njia ya kushika Sheria: “Mutu anayetimiza maagizo ya Sheria, ataishi kwa njia yake.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana Musa aieleza haki itokayo kwa sharia, akiandika ya kuwa, Mtu afanyae haya ataishi kwa haya.