Romans 10:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maandiko Matakatifu yasema hivi: “Ujumbe huo wa Mungu uko karibu nawe, uko kinywani mwako na moyoni mwako” nao ndio ile imani tunayoihubiri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini andiko lasemaje? “Lile neno liko karibu nawe, liko kinywani mwako na moyoni mwako,” yaani lile neno la imani tunalolihubiri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivi ndivyo Maandiko yanavyosema: “Mafundisho ya Mungu yako karibu nawe; yako katika kinywa chako na katika moyo wako.” Ni mafundisho ya imani tunayowaambia watu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maandiko Matakatifu yesema hivi, “Ujumbe huo wa Mungu uko karibu nawe, uko kinywani mwako na moyoni mwako” nao ndio ile imani tunayoihubiri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maandiko Matakatifu yasema hivi: “Ujumbe huo wa Mungu uko karibu nawe, uko kinywani mwako na moyoni mwako” nao ndio ile imani tunayoihubiri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini andiko lasemaje? “Lile neno li karibu nawe, li kinywani mwako na moyoni mwako,” yaani, ni lile neno la imani tunalolihubiri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini andiko lasemaje? “Lile neno liko karibu nawe, liko kinywani mwako na moyoni mwako,” yaani, lile neno la imani tunalolihubiri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini yanenaje? Lile neno liko karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maandiko Matakatifu yasema hivi: “Ujumbe huo wa Mungu uko karibu nawe, uko kinywani mwako na moyoni mwako” nao ndio ile imani tunayoihubiri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena unasema: Neno hilo linakukalia karibu, limo kinywani mwako, namo moyoni mwako. Hilo ndilo neno la kumtegemea Mungu, ni hilihili, tunalolitangaza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini inasemwa namna gani? “Neno la Mungu liko karibu nawe, liko ndani ya kinywa chako na ndani ya moyo wako.” Neno hili ni ujumbe tunaouhubiri juu ya imani.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini yasemaje? Lile neno ni karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani ni lile neno la imani tulikhubirilo;