Romans 11:12 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kosa la Wayahudi limesababisha baraka nyingi kwa ulimwengu, na utovu wao wa kiroho umeleta baraka nyingi kwa watu wa mataifa mengine. Basi, ni dhahiri kwamba kuingizwa kwa idadi yao kamili kutakuwa ni baraka zaidi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi ikiwa kukosa kwao kumekuwa utajiri mkubwa kwa ulimwengu, tena kama kuangamia kwao kumeleta utajiri kwa watu wa Mataifa, kurudishwa kwao kutaleta utajiri mkuu zaidi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, ikiwa kosa lao limekuwa utajiri wa ulimwengu, na upungufu wao umekuwa utajiri wa Mataifa, je! Si zaidi sana utimilifu wao?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kosa lao na hasara yao vilileta baraka za utajiri kwa ulimwengu kwa wasio Wayahudi. Hivyo fikirini ni kwa kiasi gani baraka hizi zitakuwa kubwa kwa ulimwengu pale idadi ya kutosha ya Wayahudi watakapokuwa watu wa aina ile anayoitaka Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kosa la Wayahudi limesababisha baraka nyingi kwa ulimwengu, na utovu wao kwa kiroho umeleta baraka nyingi kwa watu wa mataifa mengine. Basi, ni dhahiri zaidi kwamba utimilifu wao utasababisha baraka nyingi zaidi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kosa la Wayahudi limesababisha baraka nyingi kwa ulimwengu, na utovu wao wa kiroho umeleta baraka nyingi kwa watu wa mataifa mengine. Basi, ni dhahiri kwamba kuingizwa kwa idadi yao kamili kutakuwa ni baraka zaidi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi ikiwa kujikwaa kwao kumekuwa utajiri mkubwa kwa ulimwengu, tena kama kuangamia kwao kumeleta utajiri kwa watu Mataifa, kurudishwa kwao kutaleta utajiri mkuu zaidi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi ikiwa kukosa kwao kumekuwa utajiri mkubwa kwa ulimwengu, tena kama kuangamia kwao kumeleta utajiri kwa watu wa Mataifa, kurudishwa kwao kutaleta utajiri mkuu zaidi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, ikiwa kosa lao limekuwa utajiri wa ulimwengu, na upungufu wao umekuwa utajiri wa Mataifa, je! Si zaidi sana utimilifu wao?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kosa la Wayahudi limesababisha baraka nyingi kwa ulimwengu, na utovu wao wa kiroho umeleta baraka nyingi kwa watu wa mataifa mengine. Basi, ni dhahiri kwamba kuingizwa kwa idadi yao kamili kutakuwa ni baraka zaidi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini maanguko yao yakiwa yameuletea ulimwengu mapato mengi, nako kushindwa kwao kukiwa kumewaletea wamizimu mapato mengi, je? Hapo, watakapokuja wote, hayo mapato hayataongezeka sanasana?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, ikiwa kosa lao limekuwa utajiri wa ulimwengu, na upungufu wao umekuwa utajiri wa Mataifa, je! Si zaidi sana utimilifu wao?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kosa lao limeiletea dunia baraka nyingi, na upungufu wao umeleta baraka nyingi kwa watu wa mataifa mengi. Basi haitaleta baraka zaidi sana wakati Waisraeli wote watakapookoka?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
bassi ikiwa kosa lao limekuwa utajiri wa ulimwengu, na upungufu wao umekuwa utajiri wa mataifa, je! si zaidi sana utimilifu wao?