Romans 11:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana ikiwa kukataliwa kwao kulisababisha ulimwengu upatanishwe na Mungu, itakuwaje wakati watakapokubaliwa na Mungu? Wafu watafufuka!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa ikiwa kukataliwa kwao ni kupatanishwa kwa ulimwengu, kukubaliwa kwao si kutakuwa ni uhai baada ya kufa?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je! Kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si uhai baada ya kufa?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mungu aliwaacha kwa muda. Hilo lilipotokea, akawa rafiki wa watu wengine ulimwenguni. Hivyo anapowakubali Wayahudi, ni sawa na kuwafufua watu baada ya kifo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana ikiwa kukataliwa kwao kulisababisha ulimwengu upatanishwe na Mungu, itakuwaje wakati watakapokubaliwa na Mungu? Wafu watafufuka!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana ikiwa kukataliwa kwao kulisababisha ulimwengu upatanishwe na Mungu, itakuwaje wakati watakapokubaliwa na Mungu? Wafu watafufuka!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa ikiwa kukataliwa kwao ni kupatanishwa kwa ulimwengu, kukubaliwa kwao si kutakuwa ni uhai baada ya kufa?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa ikiwa kukataliwa kwao ni kupatanishwa kwa ulimwengu, kukubaliwa kwao si kutakuwa ni uhai baada ya kufa?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je! Kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si uhai baada ya kufa?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana ikiwa kukataliwa kwao kulisababisha ulimwengu upatanishwe na Mungu, itakuwaje wakati watakapokubaliwa na Mungu? Wafu watafufuka!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hapo walipotupwa waliwapatia wao wa ulimwengu wokovu; basi, hapo watakapopokelewa watawapatia nini, isipokuwa kufufuka na kutoka penye wafu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je! Kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si uhai baada ya kufa?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana ikiwa kukataliwa kwao na Mungu kumeleta upatanisho kati yake na dunia, basi si hakika kwamba kukubaliwa kwao na Mungu kutaleta uzima kwa wale waliokufa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je! kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si uhayi baada ya kufa?