Romans 11:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naam, baadhi ya matawi ya mzeituni bustanini yalikatwa, na mahali pake tawi la mzeituni mwitu likapandikizwa. Nyinyi watu wa mataifa mengine ndio hilo tawi la mzeituni mwitu; na sasa mnashiriki nguvu na utomvu wa mzeituni bustanini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kama baadhi ya matawi yalikatwa, nawe chipukizi la mzeituni mwitu ukapandikizwa mahali pao ili kushiriki unono pamoja na matawi mengine kutoka shina la mzeituni,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini iwapo matawi mengine yamekatwa, na wewe mzeituni mwitu ulipandikizwa kati yao, ukawa mshirika wa shina la mzeituni na unono wake,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ni kama vile baadhi ya matawi ya mzeituni yamevunjwa, na tawi la mzeituni mwitu limeunganishwa katika ule mti wa kwanza. Ikiwa wewe si Myahudi, uko sawa na tawi la mzeituni mwitu, na sasa unashiriki nguvu na uhai wa mti wa kwanza.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naam, baadhi ya matawi ya mzeituni bustanini yalikatwa, na mahali pake tawi la mzeituni mwitu likapandikizwa. Ninyi watu wa mataifa mengine ndio hilo tawi la mzeituni mwitu; na sasa mnashiriki nguvu na utomvu wa mzeituni bustanini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naam, baadhi ya matawi ya mzeituni bustanini yalikatwa, na mahali pake tawi la mzeituni mwitu likapandikizwa. Nyinyi watu wa mataifa mengine ndio hilo tawi la mzeituni mwitu; na sasa mnashiriki nguvu na utomvu wa mzeituni bustanini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kama baadhi ya matawi yalikatwa, nawe chipukizi la mzeituni mwitu ukapandikizwa mahali pao ili kushiriki unono pamoja na matawi mengine kutoka katika shina la mzeituni,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kama baadhi ya matawi yalikatwa, nawe chipukizi la mzeituni mwitu ukapandikizwa mahali pao ili kushiriki unono pamoja na matawi mengine kutoka shina la mzeituni,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini iwapo matawi mengine yamekatwa, na wewe mzeituni mwitu ulipandikizwa kati yao, ukawa mshirika wa shina la mzeituni na unono wake,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naam, baadhi ya matawi ya mzeituni bustanini yalikatwa, na mahali pake tawi la mzeituni mwitu likapandikizwa. Nyinyi watu wa mataifa mengine ndio hilo tawi la mzeituni mwitu; na sasa mnashiriki nguvu na utomvu wa mzeituni bustanini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kama yako matawi yaliyovunjwa na kuondolewa, kisha wewe uliye mdanzi tu ukatiwa mahali pao, ukagawiwa fungu lako la shina na utomvu wa ule mchungwa,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini iwapo matawi mengine yamekatwa, na wewe mzeituni mwitu ulipandikizwa kati yao, ukawa mshirika wa shina la mzeituni na unono wake,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Matawi mamoja ya muzeituni uliopandwa yamekatwa, na chipukizi la muzeituni uliojiotesha katika pori umepandikizwa kwenye nafasi yao. Na sasa unafaidia vilevile utomvu unaotoka ndani ya shina la yule muzeituni uliopandwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini iwapo matawi mengine yamekatiwa, na wewe mzeituni mwitu ulitiwa kati yao ukawa mshirika wa shina la mzeituni na unono wake,