Romans 11:26 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo ndipo taifa lote la Israeli litakapookolewa, kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mkombozi atakuja kutoka Siyoni, atauondoa uovu wa wazawa wa Yakobo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Israeli wote wataokolewa. Kama ilivyoandikwa: “Mkombozi atakuja kutoka Sayuni; ataondoa kutokumcha Mungu katika Yakobo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na hivyo ndivyo Israeli wote watakavyookolewa. Kama Maandiko yanavyosema, “Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; atauondoa uovu kutoka kwa wazaliwa wa Yakobo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo ndipo taifa lote la Israeli litakapookolewa, kama yesemavyo Maandiko Matakatifu: “Mkombozi atakuja kutoka Sioni, atauondoa uovu wa Yakobo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo ndipo taifa lote la Israeli litakapookolewa, kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mkombozi atakuja kutoka Siyoni, atauondoa uovu wa wazawa wa Yakobo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo Israeli wote wataokolewa kama ilivyoandikwa: “Mkombozi atakuja kutoka Sayuni; ataondoa kutokumcha Mungu katika Yakobo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Israeli wote wataokolewa. Kama ilivyoandikwa: “Mkombozi atakuja kutoka Sayuni; ataondoa kutokumcha Mungu katika Yakobo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo ndipo taifa lote la Israeli litakapookolewa, kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mkombozi atakuja kutoka Siyoni, atauondoa uovu wa wazawa wa Yakobo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo ndivyo, Waisiraeli wote watakavyookoka, kama ilivyoandikwa: Mle Sioni atatokea mponya; ndiye atakayemgeuza Yakobo, aache mabezo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na halafu taifa lote la Israeli litaokolewa kama vile inavyoandikwa katika Maandiko Matakatifu: “Mukombozi atatokea Sayuni, atakomesha uovu kati ya wazao wa Yakobo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
na hivi Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Yeye aokoae atakuja kutoka Sayuni Atamtenga Yakobo na maasi yake,