Romans 11:28 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa sababu wanaikataa Habari Njema, Wayahudi wamekuwa maadui wa Mungu, lakini kwa faida yenu nyinyi watu wa mataifa. Lakini, kwa kuwa waliteuliwa, bado ni marafiki wa Mungu kwa sababu ya babu zao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa habari ya Injili, wao ni adui wa Mungu kwa ajili yenu, lakini kuhusu kule kuteuliwa kwao ni wapendwa, kwa ajili ya baba zao wa zamani;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi kwa habari ya Injili wamekuwa adui kwa ajili yenu; bali kwa habari ya kule kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili ya baba zetu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa sasa, Wayahudi wanaokataa kuzipokea Habari Njema wamekuwa adui wa Habari Njema. Hili limetokea kwa manufaa yenu ninyi msio Wayahudi. Lakini bado Wayahudi ni wateule wa Mungu, na anawapenda kwa sababu ya ahadi alizozifanya kwa baba zao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa sababu wanaikataa Habari Njema, Wayahudi wamekuwa adui wa Mungu, lakini kwa faida yenu nyinyi watu wa mataifa. Lakini, kwa kuwa waliteuliwa, bado ni rafiki wa Mungu kwa sababu ya baba zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa sababu wanaikataa Habari Njema, Wayahudi wamekuwa maadui wa Mungu, lakini kwa faida yenu nyinyi watu wa mataifa. Lakini, kwa kuwa waliteuliwa, bado ni marafiki wa Mungu kwa sababu ya babu zao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa habari ya Injili, wao ni adui wa Mungu kwa ajili yenu, lakini kuhusu kule kuteuliwa kwao ni wapendwa, kwa ajili ya mababa zao wa zamani,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa habari ya Injili, wao ni adui wa Mwenyezi Mungu kwa ajili yenu, lakini kuhusu kule kuteuliwa kwao ni wapendwa, kwa ajili ya mababa zao wa zamani,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi kwa habari ya Injili wamekuwa adui kwa ajili yenu; bali kwa habari ya kule kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili ya baba zetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa sababu wanaikataa Habari Njema, Wayahudi wamekuwa maadui wa Mungu, lakini kwa faida yenu nyinyi watu wa mataifa. Lakini, kwa kuwa waliteuliwa, bado ni marafiki wa Mungu kwa sababu ya babu zao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hivyo, wanavyoukataa Utume mwema, ndio wachukivu kwa ajili yenu; lakini kwa hivyo, walivyochaguliwa, ndio wapendwa kwa ajili ya baba zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi kwa habari ya Injili wamekuwa adui kwa ajili yenu; bali kwa habari ya kule kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili ya baba zetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wayuda wamegeuka waadui za Mungu kwa sababu ya kukataa Habari Njema, na jambo hilo limekuwa faida kwenu ninyi watu wa mataifa mengine. Lakini wao ni wapendwa wake kufuatana na vile wamechaguliwa naye, kwa njia ya babu zao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi kwa khabari ya Injili wamekuwa adui kwa ajili yenu, bali kwa khabari ya kule kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili ya haha zetu.