Romans 11:33 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Utajiri, hekima na elimu ya Mungu ni kuu mno! Huruma zake hazichunguziki, na njia zake hazieleweki! Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tazama jinsi kilivyo kina cha utajiri wa hekima na maarifa ya Mungu! Tazama jinsi hukumu zake hazichunguziki, na ambavyo njia zake hazitafutiki!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndiyo, utajiri wa Mungu ni mkuu sana! Hekima yake na ufahamu wake havina mwisho! Hakuna awezaye kuelezea yale Mungu anayoyaamua. Hayupo awezaye kuzielewa njia zake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Utajiri, hekima na elimu ya Mungu ni kuu mno! Huruma zake hazichunguziki, na njia zake hazieleweki! Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Utajiri, hekima na elimu ya Mungu ni kuu mno! Huruma zake hazichunguziki, na njia zake hazieleweki! Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tazama jinsi kilivyo kina cha utajiri wa hekima na maarifa ya Mungu! Tazama jinsi ambavyo hukumu zake hazichunguziki, na ambavyo njia zake zisivyotafutikana!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tazama jinsi kilivyo kina cha utajiri wa hekima na maarifa ya Mungu! Tazama jinsi ambavyo hukumu zake hazichunguziki, na ambavyo njia zake zisivyotafutikana!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazieleweki!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Utajiri, hekima na elimu ya Mungu ni kuu mno! Huruma zake hazichunguziki, na njia zake hazieleweki! Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Tazameni, jinsi ujuzi na utambuzi wake Mungu unavyofurika kuwa mwingi! Kweli maamuzi yake hayachunguziki, njia zake nazo hazinyatiliki!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utajiri wa Mungu, hekima na ufahamu wake ni vikubwa kupita kipimo! Hakuna anayeweza kuvumbua kusudi lake wala kuelewa mipango yake!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ee ajabu ya utajiri na hekima na maarifa ya Mungu; hazina hatta kiasi! hukumu zake hazichunguziki, na njia zake hazitafutikani!