Romans 12:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wapenzi wangu, msilipize kisasi, bali mwachieni Mungu jambo hilo; maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kulipiza kisasi ni shauri langu; mimi nitalipiza, asema Bwana.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wapendwa, msilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa: “Ni juu yangu kulipiza kisasi, nitalipiza,” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Rafiki zangu, msijaribu kumwadhibu yeyote anayewakosea. Msubiri Mungu katika hasira yake awaadhibu. Katika Maandiko Bwana anasema, “Nitawaadhibu wao kwa ajili ya yale waliyofanya.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wapenzi wangu, msilipize kisasi, bali mwachieni Mungu jambo hilo; maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kulipiza kisasi ni shauri langu; mimi nitalipiza asema Bwana.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wapenzi wangu, msilipize kisasi, bali mwachieni Mungu jambo hilo; maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kulipiza kisasi ni shauri langu; mimi nitalipiza, asema Bwana.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wapendwa, msilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa: “Kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa, asema Bwana.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wapendwa, msilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, maana imeandikwa: “Ni juu yangu kulipiza kisasi, nitalipiza,” asema Bwana Mwenyezi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wapenzi wangu, msilipize kisasi, bali mwachieni Mungu jambo hilo; maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kulipiza kisasi ni shauri langu; mimi nitalipiza, asema Bwana.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wapendwa, msijilipize wenyewe, ila jitengeni, makali (ya Mungu) yapate kutokea! Kwani imeandikwa: Bwana anasema: Lipizi ni langu mimi, ni mimi nitakayelipisha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wandugu wapendwa, musilipize kisasi ninyi kwa ninyi, lakini mumwachie Mungu wakati wa kutenda kufuatana na kasirani, maana imeandikwa katika Maandiko Matakatifu: “Ni kazi yangu kulipiza kisasi. Ni mimi nitakayelipiza.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Msijilipize kisasi, wapenzi, bali ipisheni ghadhabu; maana imeandikwa, Kisasi juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.