Romans 12:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Msiige mitindo ya ulimwengu huu, bali Mungu afanye mabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikira zenu. Hapo ndipo mtakapoweza kuyajua mapenzi ya Mungu na kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na kamilifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kujaribu ili kuthibitisha mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza na kamilifu machoni pake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Msifikiri au kuenenda kama watu wa ulimwengu huu, bali mruhusuni Mungu aibadilishe namna yenu ya kufikiri ndani yenu. Ndipo mtaweza kuelewa na kuyathibitisha yale Mungu anayotaka kutoka kwenu; yote yaliyo mema, yanayompendeza yeye na yaliyo makamilifu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Msiige mitindo ya ulimwengu huu, bali Mungu afanye mabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikira zenu. Hapo ndipo mtakapoweza kuyajua mapenzi ya Mungu, kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na kamilifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Msiige mitindo ya ulimwengu huu, bali Mungu afanye mabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikira zenu. Hapo ndipo mtakapoweza kuyajua mapenzi ya Mungu na kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na kamilifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kuonja na kuhakikisha ni nini mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza machoni Pake na ukamilifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kuonja na kuhakikisha ni nini mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza machoni pake na ukamilifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala msifuate kanuni za dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Msiige mitindo ya ulimwengu huu, bali Mungu afanye mabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikira zenu. Hapo ndipo mtakapoweza kuyajua mapenzi ya Mungu na kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na kamilifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Msijifananishe nao walio wa siku hizi tu, ila mgeuke, mpewe mawazo mapya, mpate kuyapambanua, Mungu ayatakayo kwamba: Ni mema ya kumpendeza hapo, yatakapotimilika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musifuate mwenendo wa siku hizi, lakini muache Mungu awabadilishe kwa kugeuza upya nia zenu, hata mukuwe na mawazo mapya. Kwa hiyo mutaweza kutambua mapenzi ya Mungu. Mutajua mambo gani yanayokuwa mema, yanayomupendeza Mungu na yanayokuwa makamilifu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wala msifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufunya upya nia zenu, mpate kujua kwa hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.