Romans 12:20 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Zaidi ya hayo, Maandiko yasema: “Adui yako akiwa na njaa, mpe chakula; akiwa na kiu, mpe kinywaji. Maana kwa kufanya hivyo utamfanya apate aibu kali kama makaa ya moto juu ya kichwa chake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Badala yake: “Kama adui yako ana njaa, mlishe; kama ana kiu, mpe kinywaji. Kwa kufanya hivyo, unaweka makaa ya moto yanayowaka kichwani pake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Badala yake, “ikiwa una adui wenye njaa, wapeni chakula wale. Ikiwa wana kiu, wapeni kinywaji wanywe. Kwa kufanya hivyo mtawafanya wajisikie aibu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tena, Maandiko yasema: “Adui yako akiwa na njaa, mpe chakula; akiwa na kiu, mpe kinywaji. Maana kwa kufanya hivyo utamfanya apate aibu kali kama makaa ya moto juu ya kichwa chake.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Zaidi ya hayo, Maandiko yasema: “Adui yako akiwa na njaa, mpe chakula; akiwa na kiu, mpe kinywaji. Maana kwa kufanya hivyo utamfanya apate aibu kali kama makaa ya moto juu ya kichwa chake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Badala yake: “Adui yako akiwa na njaa, mpe chakula; akiwa na kiu, mnyweshe. Maana ukifanya hivyo, utampalia makaa ya moto yanayowaka kichwani pake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Badala yake: “Kama adui yako ana njaa, mlishe; kama ana kiu, mpe kinywaji. Kwa kufanya hivyo, unaweka makaa ya moto yanayowaka kichwani pake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Zaidi ya hayo, Maandiko yasema: “Adui yako akiwa na njaa, mpe chakula; akiwa na kiu, mpe kinywaji. Maana kwa kufanya hivyo utamfanya apate aibu kali kama makaa ya moto juu ya kichwa chake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mchukivu wako akiwa ana njaa, mpe chakula! Akiwa ana kiu, mpe cha kunywa! Kwani ukivifanya hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kama vile Maandiko Matakatifu yanavyosema: “Adui yako akisikia njaa, umupe chakula; kama akisikia kiu, umupe kinywaji. Maana kwa kufanya hivi utamupatisha haya kama vile ungemubebesha makaa ya moto juu ya kichwa.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivi, utampalia makaa ya moto kichwani pake.