Romans 13:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Msiwe na deni kwa mtu yeyote, isipokuwa tu deni la kupendana. Ampendaye jirani yake ameitekeleza sheria.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Msidaiwe kitu na mtu yeyote, isipokuwa kupendana, kwa maana yeye ampendaye mwenzake, ameitimiza sheria.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Msidaiwe chochote na mtu, isipokuwa mdaiwe upendo baina yenu. Mtu anayewapenda wengine anakuwa amefanya yote yanayoamriwa na sheria.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Msiwe na deni kwa mtu yeyote, isipokuwa tu deni la kupendana. Ampendaye jirani yake ameitekeleza Sheria.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Msiwe na deni kwa mtu yeyote, isipokuwa tu deni la kupendana. Ampendaye jirani yake ameitekeleza sheria.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Msidaiwe kitu na mtu ye yote, isipokuwa kupendana, kwa maana yeye ampendaye mwenzake, ameitimiza Sheria.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Msidaiwe kitu na mtu yeyote, isipokuwa kupendana, kwa maana yeye ampendaye mwenzake, ameitimiza sheria.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Msiwiwe na mtu chochote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Msiwe na deni kwa mtu yeyote, isipokuwa tu deni la kupendana. Ampendaye jirani yake ameitekeleza sheria.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Msiwe wadeni wa mtu ye yote, isipokuwa wa kupendana! Kwani anayempenda mwenziwe ameyatimiza Maonyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musikuwe na deni la mutu yeyote. Deni moja munalopaswa kuwa nalo ni kupendana. Kwa maana yule anayemupenda mwenzake ametimiza Sheria kabisa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendae mtu mwenzake ameitimiza sharia.