Romans 13:9 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana, amri hizi: “Usizini; Usiue; Usitamani;” na nyingine zote, zimo katika amri hii moja: “Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa amri hizi zisemazo, “Usizini,” “Usiue,” “Usiibe,” “Usitamani,” na amri nyingine zote, zinajumlishwa katika amri hii moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sheria inasema, “Usizini, usiue, usiibe, usitamani kitu cha mtu mwingine.” Amri hizo zote na zingine hakika zinajumlishwa na kuwa kanuni moja tu, “Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana, amri hizi: “Usizini; Usiue; Usitamani;” na nyingine zote, zimo katika amri hii moja: “Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana, amri hizi: “Usizini; Usiue; Usitamani”; na nyingine zote, zimo katika amri hii moja: “Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa amri hizi zisemazo, “Usizini,” “Usiue,” “Usiibe,” “Usitamani,” na amri nyingine zote, zinajumlishwa katika amri hii moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa amri hizi zisemazo, “Usizini,” “Usiue,” “Usiibe,” “Usitamani,” na amri nyingine zote, zinajumlishwa katika amri hii moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yoyote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana, amri hizi: “Usizini; Usiue; Usitamani;” na nyingine zote, zimo katika amri hii moja: “Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani kule kwamba: Usizini! Usiue! Usiibe! Usishuhudie uwongo! Usitamani! na kama liko agizo jingine, yanaunganika yote katika neno hili: Umpende mwenzio, kama unavyojipenda mwenyewe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo amri hizi: “Usizini, usiue, usiibe, usitamani,” pamoja na zingine zote, zinafungwa katika amri hii moja: “Umupende mwenzako sawa vile unavyojipenda mwenyewe.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana ile, Usizini, Usiue, Usiibe, Usishududu uwongo, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani wako kama nafsi yako.