Romans 14:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, tuache kuhukumiana, bali tuazimie kutokuwa kamwe kikwazo kwa ndugu au kumsababisha aanguke katika dhambi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo tusiendelee kuhukumiana. Badala yake mtu aamue kutoweka kamwe kikwazo au kizuizi katika njia ya ndugu mwingine.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi tusizidi kuhukumiana, bali afadhali toeni hukumu hii, mtu asitie kitu cha kumkwaza ndugu au cha kumwangusha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo tuache kuhukumiana sisi kwa sisi. Tuamue kutokufanya kitu ambacho kitasababisha matatizo kwa kaka au dada au kuathiri imani zao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, tuache kuhukumiana, bali tuazimie kutokuwa kamwe kikwazo kwa ndugu yetu au kumsababisha aanguke katika dhambi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, tuache kuhukumiana, bali tuazimie kutokuwa kamwe kikwazo kwa ndugu au kumsababisha aanguke katika dhambi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo tusiendelee kuhukumiana: Badala yake mtu asiweke kamwe kikwazo au kizuizi katika njia ya mwingine.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo tusiendelee kuhukumiana: Badala yake mtu asiweke kamwe kikwazo au kizuizi katika njia ya ndugu mwingine.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi tusiendelee kuhukumiana, bali amueni kuwa mtu asifanye kitu cha kumkwaza ndugu au cha kumwangusha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, tuache kuhukumiana, bali tuazimie kutokuwa kamwe kikwazo kwa ndugu au kumsababisha aanguke katika dhambi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, tusiumbuane wenyewe tena, ila mjue, ya kuwa ni kuumbua, mtu akimtegea ndugu yake, ajigonge au ajikwae!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi tusizidi kuhukumiana, bali afadhali toeni hukumu hii, mtu asitie kitu cha kumkwaza ndugu au cha kumwangusha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi tusihukumiane tena sisi wenyewe. Lakini tafazali mukamate kusudi hili: mutu asifanye kitu kinachoweza kumukwaza au kumwangusha ndugu yake katika zambi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi tusizidi kuhukumiana, bali afadhali mtoe hukumu hii, ndugu asitiwe kitu cha kumkwaza au cha kumwangusha.