Romans 14:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, shikilia unachoamini kati yako na Mungu wako. Heri mtu yule ambaye, katika kujiamulia la kufanya, haipingi dhamiri yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, wewe unayo imani? Ile imani uliyo nayo, uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Heri mtu yule asiye na sababu ya kujihukumu nafsi yake kwa ajili ya kile anachokifanya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ile imani uliyo nayo uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Heri mtu yule asiyejihukumu nafsi yake katika neno lile analolikubali.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ilindeni imani yenu kuhusu mambo haya kama siri kati yenu na Mungu. Ni baraka kufanya kile unachofikiri ni sahihi bila kujihukumu mwenyewe.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, shikilia unachoamini kati yako na Mungu wako. Heri mtu yule ambaye, katika kujiamulia la kufanya, haipingi dhamiri yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, shikilia unachoamini kati yako na Mungu wako. Heri mtu yule ambaye, katika kujiamulia la kufanya, haipingi dhamiri yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, wewe unayo imani? Ile imani uliyo nayo, uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Heri mtu yule asiye na sababu ya kujihukumu nafsi yake kwa ajili ya kile anachokifanya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, wewe unayo imani? Ile imani uliyo nayo, uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Heri mtu yule asiye na sababu ya kujihukumu nafsi yake kwa ajili ya kile anachokifanya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ile imani uliyo nayo uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Heri mtu yule asiyejihukumu nafsi yake katika neno lile analolikubali.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, shikilia unachoamini kati yako na Mungu wako. Heri mtu yule ambaye, katika kujiamulia la kufanya, haipingi dhamiri yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wewe unayoyategemea moyoni, yategemee hata mbele ya Mungu! Mwenye shangwe ni yule asiyejipatia hukumu kwa ajili yao yale, aliyoyaona kuwa ya kufaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ile imani uliyo nayo uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Heri mtu yule asiyejihukumu nafsi yake katika neno lile analolikubali.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ulinde kwa ajili yako mwenyewe kile unachoaminia juu ya mambo yale mbele ya Mungu. Heri mutu asiyejihukumu katika kusudi lake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Je! unayo imani? Uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Yu kheri mtu yule asiyejihukumu katika neno lile alikubalilo.