Romans 14:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini mtu anayeona shaka juu ya chakula anachokula, anahukumiwa kama akila, kwa sababu msimamo wa kitendo chake haumo katika imani. Na, chochote kisicho na msingi wake katika imani ni dhambi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kama mtu ana shaka kuhusu kile anachokula, amehukumiwa, kwa sababu hakula kwa imani. Kwa kuwa chochote kinachofanywa pasipo imani ni dhambi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini ikiwa unakula kitu bila kuwa na uhakika kuwa ni sahihi, unakosea. Hii ni kwa sababu hukuamini kuwa ni sahihi. Na ukifanya chochote unachoamini kuwa si sahihi, hiyo ni dhambi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini mtu anayeona shaka juu ya chakula anachokula, anahukumiwa kama akila, kwa sababu msimamo wa kitendo chake haumo katika imani. Na, chochote kisicho na msingi wake katika imani ni dhambi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini mtu anayeona shaka juu ya chakula anachokula, anahukumiwa kama akila, kwa sababu msimamo wa kitendo chake haumo katika imani. Na, chochote kisicho na msingi wake katika imani ni dhambi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kama mtu ana shaka kuhusu kile anachokula, asile hicho kitu, kwa sababu hakula kwa imani. Kwa kuwa cho chote kinachofanywa pasipo imani ni dhambi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kama mtu ana shaka kuhusu kile anachokula, amehukumiwa, kwa sababu hakula kwa imani. Kwa kuwa chochote kinachofanywa pasipo imani ni dhambi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini aliye na mashaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini mtu anayeona shaka juu ya chakula anachokula, anahukumiwa kama akila, kwa sababu msimamo wa kitendo chake haumo katika imani. Na, chochote kisicho na msingi wake katika imani ni dhambi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mtu akila mwenye mashaka amekwisha kujipatia hukumu, kwani hakula kwa kumtegemea Mungu. Nayo yote, mtu anayoyafanya pasipo kumtegemea Mungu, ndiyo makosa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mutu anayekuwa na mashaka juu ya chakula anachokula, Mungu anamuhukumu, kwa sababu hatendi kufuatana na imani. Na kitendo chochote kisichotokana na imani ni zambi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini aliye na mashaka, kama akila, amehukumiwa, kwa maana hakula kwa imani. Na killa tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.