Romans 14:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wewe ni nani hata uthubutu kumhukumu mtumishi wa mwingine? Akisimama au akianguka ni shauri la Bwana wake; naam, atasimama imara, maana Bwana anaweza kumsimamisha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wewe ni nani hata umhukumu mtumishi wa mtu mwingine? Kwa bwana wake tu anasimama au kuanguka. Naye atasimama kwa sababu Bwana anaweza kumsimamisha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wewe u nani unayemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa bwana wake mwenyewe yeye husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, kwa kuwa Bwana aweza kumsimamisha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Huwezi kuwahukumu watumishi wa mtu mwingine. Hilo linamhusu bwana wao mwenyewe ikiwa watafaulu au watashindwa. Na watakubaliwa, kwa sababu Bwana yuko tayari kuwafanya wafaulu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wewe ni nani hata uthubutu kumhukumu mtumishi wa mwingine? Akisimama au akianguka ni shauri la Bwana wake; naam, atasimama imara, maana Bwana anaweza kumsimamisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wewe ni nani hata uthubutu kumhukumu mtumishi wa mwingine? Akisimama au akianguka ni shauri la Bwana wake; naam, atasimama imara, maana Bwana anaweza kumsimamisha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wewe ni nani hata umhukumu mtumishi wa mtu mwingine? Kwa bwana wake tu anasimama au kuanguka. Naye atasimama kwa sababu Bwana anaweza kumsimamisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wewe ni nani hata umhukumu mtumishi wa mtu mwingine? Kwa bwana wake tu anasimama au kuanguka. Naye atasimama kwa sababu Bwana Isa anaweza kumsimamisha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wewe u nani unayemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa bwana wake mwenyewe yeye husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, kwa kuwa Bwana aweza kumsimamisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wewe ni nani hata uthubutu kumhukumu mtumishi wa mwingine? Akisimama au akianguka ni shauri la Bwana wake; naam, atasimama imara, maana Bwana anaweza kumsimamisha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wewe u nani ukimwumbua mtumishi wa mwingine? Akiwa amesimama au akiwa ameanguka, yote humfanyizia Bwana wake mwenyewe. Lakini atainuliwa, kwani Bwana anaweza kumwinua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wewe u nani unayemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa bwana wake mwenyewe yeye husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, kwa kuwa Bwana aweza kumsimamisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe ni nani unayehukumu mutumishi wa mwingine? Akisimama imara katika kazi yake au akianguka, hilo ni shauri la bwana wake. Naye atasimama imara maana Bwana yuko na uwezo wa kumusimamisha.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wewe u nani unaemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa Bwana wake mwenyewe husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, maana Bwana aweza kumsimamisha.