Romans 14:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Anayeadhimisha siku fulani anaadhimisha siku hiyo kwa ajili ya kumtukuza Mungu; naye anayekula chakula fulani anafanya hivyo kwa kumtukuza Bwana maana anamshukuru Mungu. Kadhalika naye anayeacha kula chakula fulani anafanya hivyo kwa ajili ya kumtukuza Bwana, naye pia anamshukuru Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeye anayehesabu siku moja kuwa takatifu kuliko nyingine, hufanya hivyo kwa kumheshimu Mwenyezi Mungu. Naye alaye nyama hula kwa Mwenyezi Mungu, kwa maana humshukuru Mungu, naye akataaye kula nyama hufanya hivyo kwa Mwenyezi Mungu na humshukuru Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wale wanaofikiri kuwa siku moja ni ya muhimu kuliko siku zingine wanafanya hivyo kwa ajili ya Bwana. Na wale wanaokula vyakula vya aina zote wanafanya hivyo kwa ajili ya Bwana. Ndiyo, wanamshukuru Mungu kwa ajili ya chakula. Na wale wanaokataa kula vyakula fulani wanafanya hivyo kwa ajili ya Bwana. Nao pia wanamshukuru Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Anayeadhimisha siku fulani anaadhimisha siku hiyo kwa ajili ya kumtukuza Mungu; naye anayekula chakula fulani anafanya hivyo kwa kumtukuza Bwana maana anamshukuru Mungu. Kadhalika naye anayeacha kula chakula fulani anafanya hivyo kwa ajili ya kumtukuza Bwana, naye pia anamshukuru Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Anayeadhimisha siku fulani anaadhimisha siku hiyo kwa ajili ya kumtukuza Mungu; naye anayekula chakula fulani anafanya hivyo kwa kumtukuza Bwana maana anamshukuru Mungu. Kadhalika naye anayeacha kula chakula fulani anafanya hivyo kwa ajili ya kumtukuza Bwana, naye pia anamshukuru Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yeye anayehesabu siku moja kuwa takatifu kuliko nyingine, hufanya hivyo kwa kumheshimu Bwana. Naye alaye nyama hula kwa Bwana, kwa maana humshukuru Mungu, naye akataaye kula nyama hufanya hivyo kwa Bwana na humshukuru Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeye anayehesabu siku moja kuwa takatifu kuliko nyingine, hufanya hivyo kwa kumheshimu Mwenyezi Mungu. Naye alaye nyama hula kwa Bwana Isa, kwa maana humshukuru Mwenyezi Mungu, naye akataaye kula nyama hufanya hivyo kwa Bwana Isa na humshukuru Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Anayeadhimisha siku fulani anaadhimisha siku hiyo kwa ajili ya kumtukuza Mungu; naye anayekula chakula fulani anafanya hivyo kwa kumtukuza Bwana maana anamshukuru Mungu. Kadhalika naye anayeacha kula chakula fulani anafanya hivyo kwa ajili ya kumtukuza Bwana, naye pia anamshukuru Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Anayezishika siku humshikia Bwana; naye asiyezishika hazishiki kwa ajili yake Bwana. Naye anayekula humlia Bwana, kwani humshukuru Mungu. Naye asiyekula hali kwa ajili yake Bwana, maana naye humshukuru Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu yeyote anayeshugulika juu ya siku fulani, anafanya hivi kwa kumutukuza Bwana. Yule anayekula kila chakula, anafanya vile kwa kumutukuza Bwana; maana anamushukuru Mungu kwa ajili ya chakula chake. Na asiyekula kila chakula anafanya hivi vilevile kwa kumutukuza Bwana na kumushukuru Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yeye aadhimishae siku, kwa Bwana aiadhimisha; na yeye asiyeadhimisha siku, haiadhimishi kwa Bwana; nae alae, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; nae asiokula, hali kwa Bwana, nae amshukuru Mungu.