Romans 15:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
ya kuwa mtumishi wa Yesu Kristo kwa watu wa mataifa. Ni jukumu langu la kikuhani kuihubiri Habari Njema ya Mungu ili watu wa mataifa mengine wapate kuwa tambiko inayokubaliwa na Mungu, tambiko iliyotakaswa na Roho Mtakatifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
niwe mhudumu wa Al-Masihi Isa kwa watu wa Mataifa. Alinipa huduma ya kikuhani ya kutangaza Injili ya Mungu, ili watu wa Mataifa wapate kuwa dhabihu inayokubalika na Mungu, kwa kutakaswa na Roho wa Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ili niwe mhudumu wa Kristo Yesu kati ya watu wa Mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi Mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
kuwa mtumishi wa Kristo Yesu kwa ajili ya wasio Wayahudi. Natumika kama kuhani ambaye kazi yake ni kuhubiri Habari Njema kutoka kwa Mungu. Alinipa mimi jukumu hili ili ninyi msio Wayahudi mweze kuwa sadaka atakayoikubali, sadaka iliyotakaswa na Roho Mtakatifu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
ya kuwa mtumishi wa Yesu Kristo kwa watu wa mataifa. Ni jukumu langu la kikuhani kuihubiri Habari Njema ya Mungu ili watu wa mataifa mengine wapate kuwa dhabihu inayokubaliwa na Mungu, dhabihu iliyotakaswa na Roho Mtakatifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
ya kuwa mtumishi wa Yesu Kristo kwa watu wa mataifa. Ni jukumu langu la kikuhani kuihubiri Habari Njema ya Mungu ili watu wa mataifa mengine wapate kuwa tambiko inayokubaliwa na Mungu, tambiko iliyotakaswa na Roho Mtakatifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ili kuwa mhudumu wa Kristo Yesu kwa watu Mataifa nikiwa na huduma ya kikuhani ya kutangaza Injili ya Mungu, ili watu Mataifa wapate kuwa dhabihu inayokubaliwa na Mungu, iliyotakaswa na Roho Mtakatifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ili kuwa mhudumu wa Al-Masihi Isa kwa watu wa Mataifa nikiwa na huduma ya kikuhani ya kutangaza Injili ya Mungu, ili watu wa Mataifa wapate kuwa dhabihu inayokubaliwa na Mungu, iliyotakaswa na Roho wa Mwenyezi Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ili niwe mhudumu wa Kristo Yesu kati ya watu wa Mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi Mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
ya kuwa mtumishi wa Yesu Kristo kwa watu wa mataifa. Ni jukumu langu la kikuhani kuihubiri Habari Njema ya Mungu ili watu wa mataifa mengine wapate kuwa tambiko inayokubaliwa na Mungu, tambiko iliyotakaswa na Roho Mtakatifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nimtumikie Kristo Yesu nikiwatangazia wamizimu Utume mtakatifu wa Mungu na kuwaombea, kusudi wawe kipaji cha tambiko kipendezekacho, kwa kuwa kimetakaswa katika Roho Mtakatifu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ili niwe mhudumu wa Kristo Yesu kati ya watu wa Mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi Mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kuwa mutumishi wa Yesu Kristo kwa watu wa mataifa mengine. Ninafanya kazi ya ukuhani ya kuhubiri Habari Njema ya Mungu, kusudi watu wa mataifa mengine wapate kuwa kama sadaka inayokubaliwa na Mungu na iliyotakaswa na Roho Mutakatifu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
illi niwe kuhani wa Yesu Kristo katika watu wa mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu.